August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mdee kutupwa mahabusu kwa saa 48

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe

Spread the love

ALLY Hapi, Mkuu wa Wilaya Kinondoni,  amemuagiza Suzan Kaganda, Kamanda wa Polisi  wa Kinondoni (RPC) kumkamata Halima Mdee, Mbunge wa Kawe kutokana na kutoa maneno ya uchochezi kwa Rais John Magufuli, anaandika Hamisi Mguta.

Hapi ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizungumza na wanahabari ofisini kwake ambapo amemtaka RPC Kaganda kumweka mahabusu kwa saa 48.

Mdee anadaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na ya uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) uliofanyika jana makao makuu ya chama hicho.

Hapi kuwa amesema kauli za Mdee kuhusu wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni, imemshtua yeye kama mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo.

“Maneno yake ni ya kichochezi ambayo hayakubaliki, hayafai kutolewa na kiongozi kama yeye hivyo namuagiza kamanda amkamate Mdee amweke ndani kwa saa 48 ili ahojiwe yale yote aliyoyaongea ili afikishwe kwenye vyombo vya usalama,”amesema.

Hata hivyo, Henry Kilewo amesema Mdee amekamatwa na Polisi na Kupekekwa kituoni Oysterbay.

error: Content is protected !!