August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge wa Chadema wahojiwa Polisi

Wabunge wa Chadema waliohojiwa kwa tuhuma za kumshambulia Juliana Shonza, Mbunge wa Viti Maalum CCM

Spread the love

BAADA ya wabunge nane wa Chadema kukamatwa na kuachiwa kwa dhamana jana usiku, leo wametakiwa kuripoti Polisi mjini Dodoma kwa mahojiano zaidi, anaandika Hellen Sisya.

Wabunge hao walishikiliwa na Polisi kwa makosa ya kudhuru mwili yaliyoripotiwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza muda mchache baada ya pande hizo mbili kulumbana nje ya jengo la Bunge.

Wabunge wa Chadema ambao wanaohojiwa na Polisi ni pamoja na Joseph Selasini, Suzan Kiwanga, Saed Kubenea, Cecilia Pareso,  Francis Mwakajoka na Pauline Gekul.

Sakata hilo lilitokea baada ya wabunge wa Chadema kukutana na Shonza na kumwambia anachikifanya bungeni inatokana na chuki zake na upinzani, hali iliyosababisha naye kujibu mapigo na kuzua mvutano.

Shonza alichangia bungeni alikaririwa akiwasil;isha mapendekezo ya kuongezewa adhabu kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa lengo la kuendelea kukaa nje ya bunge na ikiwezekana kuongezewa adhabu zaidi.

MwanaHALISI Online itakupa taarifa zaidi kuhusiana na mahojiano hayo yanayoendelea mjini Dodoma.

error: Content is protected !!