Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kiwango cha chini cha uhuru habari China chaongeza mashaka
Kimataifa

Kiwango cha chini cha uhuru habari China chaongeza mashaka

Spread the love

 

RIPOTI ya waandishi wa Habari wasiokuwa na mipaka duniani wanaosimamia tovuti ya ‘Just Earth News’ iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu inaiweka China kuwa kwenye nafasi pili kwenye nchi zisizo kuwa na uhuru wa habari duniani ikizidiwa na Korea Kaskazini, Imeripotiwa na Business Standard …(endelea).

Ripoti hiyo kuwa waandishi wa habari na hata raia hawako salama ambapo wengine huchunguzwa na Chama tawala cha Kikomunisti cha China (CCP).

Tarehe 3 Mei inatambulika kimataifa kama Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ukumbusho ulioanzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1993.

Azimio la Ulimwengu la Haki za Kibinadamu, lililoidhinishwa na UN, linakubali uhuru wa kujieleza kuwa haki ya msingi ambayo inaunda msingi wa kufurahia haki nyingine za binadamu.

Kuripoti ukweli ni gharama ndani ya China. Wakosoaji kama Fang Bin, Zhang Zhan, na Li Wenliang, ambao walifichua habari muhimu kuhusu janga la COVID katika hatua zake za awali, wanaendelea kuteswa wakiwa kizuizini na Serikali ya China.

Fang Bin, ambaye aliandika ukweli wa COVID-19, aliachiliwa kutoka gerezani Aprili 30 mwaka huu lakini anajikuta hawezi kurejea nyumbani kutokana na vitisho vilivyopokelewa na familia yake huko Wuhan. Bado Mamlaka zinamfuatilia Mwenendo wake.

Fung alifungwa kimyakimya hukumu ya kutumikia miaka mitatu jela tangu mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!