Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Kitita cha NHIF kuanza Ijumaa, kuwapa wanachama nafuu zaidi
AfyaTangulizi

Kitita cha NHIF kuanza Ijumaa, kuwapa wanachama nafuu zaidi

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga
Spread the love

 

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetangaza kuanza kutumika kwa maboresho mapya ya Kitita cha Mafao kwa wanachama ambapo yatataanza rasmi siku ya Ijumaa ya tarahe 1 Machi, 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akitangaza kuanza kwa maboresho hayo, leo tarehe 28  Februari, 2024 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema Kitita cha Mafao ni orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na zitakuwa kwa bei nafuu zaidi ya hapo awali.

Konga amefafanua kuwa katika maboresho ya mwisho ya Kitita cha Mafao kinachotumika sasa yalifanyika Juni, 2016 lakini kwa kuzingatia hali ya maisha pamoja na maoni mbalimbali ya wadau wamelazimika kufanya maboresho hayo mapya.

“Ni takribani miaka nane sasa, hivyo kuwepo umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama na kuongeza huduma ambazo hazikuwepo,” amesema Konga.

Amesema, miongoni mwa manufaa ya kitita ni pamoja na wanachama wanaotumia dawa za shinikizo la damu na sukari sasa wanaweza kupata dawa ngazi za chini lakini pia wanachama wanaopata huduma ya uchujaji damu gharama imeshushwa chini.

“Na huduma za kibingwa na bingwa bobezi kama matibabu ya moyo, saratani, figo zitapatikana kwenye ngazi za kanda pia na sio lazima mwanachama aende mpaka hospitali za ngazi taifa,” amesema Konga.

Konga amesema katia maboresho hayo NHIF wameongeza aina mpya za dawa zaidi 247 kwenye kitita, hivyo kumfanya mnufaika wa mfuko huyo kutokutana na changamoto ya kukosa dawa katika kituo chochote atakachoenda kupata huduma.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga (hayupo pichani)

Amesema maboresho hayo pia yamekuja na nafuu kwa wanufaika wa mfuko huwa katika gharama za ushauri, dawa na matibabu.

Konga amesema gharama za maboresho hayo hazimgusi mwanachama bali ni kati ya NHIF na watoa huduma ili kuboresha zaidi huduma karibu na wananchi nchini.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema, maeneo muhimu yaliyofanyiwa maboresho ili kuleta unafuu huo wa gharama ni ada ya usajili na ushauri wa daktari huduma za dawa na tiba za upasuaji na vipimo.

Konga ameongeza kuwa, mfuko huo unaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau kuhusu kitita hicho na pale maboresho yatakapofanyika wataendelea kutoa taarifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!