Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kisa video iliyomuumbua Rais akijisaidia haja ndogo hadharani, waandishi habari 6 mbaroni
Kimataifa

Kisa video iliyomuumbua Rais akijisaidia haja ndogo hadharani, waandishi habari 6 mbaroni

Spread the love

WAANDISHI habari kadhaa wamekamatwa nchini Sudan Kusini baada ya kusambaa video inayomuonesha Rais wa nchi hiyo Salva Kiir yumkini akishindwa kujizuia haja ndogo kwenye hafla rasmi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jumuiya ya waandishi habari ya Sudan Kusini imetoa wito wa kufanyika uchunguzi haraka kuhusu tukio hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Video hiyo iliyotolewa na Shirika la Taifa la Utangazaji la Sudan imemwonesha Rais Kiir mwenye umri wa miaka 72 akilowesha suruali yake wakati wimbo wa taifa ukipigwa kwenye sherehe ya ufunguzi katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.

Waandishi hao sita walikamatwa baada ya video husika kuanza kusambaa.

Waliotiwa mbaroni ni pamoja na mkurugenzi wa kitengo cha udhibiti, mhariri wa maudhui, wapiga picha kadhaa na mafundi waliokuwapo wakati rais huyo akipigwa picha.

Wizara ya habari imesema waandishi hao wanasaidia katika juhudi za uchunguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!