November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa machinga kuuza senene ndani ya ndege, waziri awatimua wafanyakazi

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi na Usafirishaji nchini Uganda, Jenerali Edward Wamala ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Uganda baada ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mmoja wa wamachinga nchini humo akiwauzia senene abiria ndani ya ndege ya shirika hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Video hiyo iliyoanza kusambaa jana tarehe 27 Novemba, 2021 imemuonesha mwanaume huyo ambaye bado hajafahamika jina akiwauzia kitowea hicho abiria.

Mmachinga huyo ambaye pia haijafahamika nani alimrekodi video hiyo, alikuwa amewahifadhi senene hao kwenye mfuko wa bluu na kuwauzia abiria waliokuwa wamekaa kwenye daraja la kawaida.

“Ni Shilinga za Uganda 10,000 (sawa na Shilingi za kitanzani 6,400 )” alisikika mwanaume huyo akiwatangazia abiria waliokuwa wamekaa katika ndege hiyo aina ya Airbus A330.

Waziri wa Ujenzi na Usafirishaji nchini Uganda, Jenerali Edward Wamala

Baadhi ya watu waliokaribu na Waziri huyo wameuleza mtandao wa Chimpreport kwamba, kiongozi huyo amekasirika kutokana na tukio hilo ambalo amesema ni la kutia aibu.

Hata hivyo, haijaelezwa ni wafanyakazi wangapi wamesimamishwa kazi, lakini tukio hilo limeibua mjadala mkubwa nchini humo.

Senene ni kitoweo pendwa katika ukanda wa Kagera na maeneo yanayozunguka mkoa huo uliojirani na nchi ya Uganda

error: Content is protected !!