Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania, Uganda zakubaliana mambo saba, ‘Bomba la mafuta chakula kipo mezani’
Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uganda zakubaliana mambo saba, ‘Bomba la mafuta chakula kipo mezani’

Spread the love

 

SERIKALI za Tanzania na Uganda zimekubaliana mambo saba katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uhusiano pamoja na ushirikiano wa nchi hizo mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27 Novemba, 2021 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mambo waliyokubaliana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Rais Museveni ametua nchini leo kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atakwenda Geita kuzindua shule ya msingi Museveni iliyojengwa kwa fedha za Serikali ya Uganda.

Aidha, mbali na Rais Samia kumshukuru Rais Museveni kwa kukubali mwaliko wake, amesema hatua hiyo ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa serikali zote mbili katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa masilahi ya pande zote mbili.

“Nimshukuru kwa kukubali mwaliko wangu na kuja kufanya ziara ya kitaifa, waswahili husema raha ya udugu ni kutembeleana, nakushukuru sana Rais kwa kuja kunitembelea mdogo wako,” amesema.

Aidha akizungumzia mambo waliyojadili amesisitiza kuwa ni uhusiano na ushirikiano hasa ikizingatiwa Tanzania na Uganda sio jirani bali ni marafiki na ndugu.

Amesema katika suala hilo wamewaagiza mawaziri wa sekta kukutana mara kwa mara kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao na kuhakikisha ushirikiano huu unaendelea kuimarika.

“Pili tumezungumzia ushirikiano katika sekta ya uwekezaji, ambapo Uganda ni nchi ya pili kwa uwekezaji nchini Tanzania katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

“Uganda imewekeza jumla ya miradi 45 yenye thamani dola za Marekani milioni 114 ambayo imetoa ajira kwa Watanzania 2,150. Aidha, zipo kampuni mbalimbali za Tanzania kama Azam tv, Coseke, Bakhresa Grand Milling na nyingine.

“Mnaweza kuona uwekezaji unakwenda pande zote mbili ila tumekubaliana kuna haja ya kuongeza uwekezaji wafanyabiashara wetu kuwekeza ndani ya nchi zetu na tumewahakikisha usalama wa uwekezaji wao,” amesema.

Tatu, ni ushirikiano wa biashara ambapo Rais Samia amesema katika kipindi cha miaka saba biashara kati ya nchi hizi mbili, umeendelea kukua.

Amesema ujazo wa biashara kati ya Tanzania na Uganda, umeongezeka kutoka Sh bilioni 200 mwaka 2014 hadi bilioni 607 mwaka 2020.

“Hivyo, tumekubaliana namna ya kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi zetu mbili. Nchi zetu bado zina fursa za biashara katika sekta za viwanda, kilimo, uvuvi huduma za kijamii, utalii, usafirishaji.

“Kwa lengo lakuimarisha biashara kati yetu tumekubaliana kuondoa vikwazo visivyokuwa vya kodi hivyo tumewaelekeza mawaziri kati ya nchi hizi mbili kukutana ndani ya miezi miwili kutatua vikwazo hivyo,” amesema.

Rais Yoweri Museven

Pia wamezungumza matumizi ya bandarini ya Dar es Salaam, ambapo Rais Museveni alisema hii ni aibu kwamba hadi leo bandari ya Dar es Salaam imefikia kusafirisha tani 138,262 kwenda Uganda, wakati wanatumia bandari nyingine kwa mamilioni ya tani.

“Hivyo tumekubaliana kuongeza mzigo unaotoka Dar es Salaa kwenda Uganda.

“Pia nimemuomba aridhie kupitisha shehena ya vifaa na mizigo vitakavyotumika kwenye ujezni wa bomba la mafuta vipitie kupitia bandari ya Dar es Salaam.

“Kwenye bandari pia tumemuomba Rais Museveni aruhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wakafungue ofisi pale Kampala ili kurahisisha utendaji na ufanyaji kazi wa bandari kwa wafanyabiashara wa Uganda. Nalo amelipokea kwa mikono mwili na amekubali kuwezesha hilo,” amesema Rais Samia.

Suala lingine ni utekelezaji wa miradi ya kimkakati kama vile barabara zinazoiunganisha Tanzania, Uganda na nchi jirani pamoja na miradi ya umeme ambayo inatakelezwa kwa pamoja.

“Tumekubaliana kuongeza jitihada ili miradi hii tuenda kuijenga na tuimalize na kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na upatikanaji wa umeme katika maeneo yetu ya pembeni za mipaka ili watu waendelee kufanya kazi zao za kiuchumi,” amesema.

Rais Samia Suluhu Hassan

Kuhusu mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga – Tanzania, Rais Samia amesema Mei mwaka huu Serikali zote mbili zilikamilisha kusaini mkataba mbalimbali ya mradi huo na sasa wameridhika kuwa utekelezaji unaendelea vizuri.

Rais Samia amesema pia wamekubaliana kushirikiana katika kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha chanjo za Uviko-19, chanjo nyingine na za wanyama.

Kwa upande wake Rais Museve amesisitiza kuwa katika suala la ujenzi wa bomba hilo, kilichokuwa kinachelewesha ni uundwaji wa bomba hilo nje ya nchi badala ya ndani ya ardhi ya Tanzania au Uganda ili kuzalisha ajira na kuongeza kipato.

Hata hivyo, alifafanua kwamba baada ya majadiliako ya muda mrefu, ni kwamba bomba hilo lenye thamani ya Dola za Marekani milioni 13,00, litakunjwa nje ya nchi hizo, lakini litakuja kupakwa rangi na kuchomelewa hapa nchini gharama ambazo zitagharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni 900.

Amesema kwa kuwa zaidi ya robo tatu ya gharama za bomba hilo zitafanyika ndani ya nchi hizi mbili, hivyo kuanzia muda wowote ujenzi wake utaanza na kusisitiza kuwa chakula sasa tayari kipo mezani.

1 Comment

  • Asante sana kwa taarifa nzuri za uwekezaji.

    Jifunze Uwekezaji kwenye ardhi na majengo kwa kutembelea mtandao wa….

    UWEKEZAJI MAJENGO BLOG

    Karibuni sana.

    Rafiki yako,

    Aliko Musa.

    Real Estate Consultant.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!