KIONGOZI wa kijeshi nchini Guinea, Kanali Mamady Doumbouya anatarajiwa kuapishwa leo tarehe 1 Oktoba 2021kama rais wa mpito. Anaripoti Patricia Kighono, TUDARCo … (endelea).
Sherehe ya kuapishwa kwake itafanyika katika ikulu ya rais na kuhudhuriwa na watu walioalikwa pekee.
Kanali Doumbouya aliongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Alpha Condé mapema mwezi uliopita.
Kiongozi huyo wa kijeshi mwenye umri wa miaka 41, anatarajiwa kuunda serikali katika wiki chache zijazo.
Doumbouya atakuwa kiongozi wa pili wa Barani Afrika mwenye umri mdogo kuongoza nchi, mdogo zaidi akiwa ni wa Mali, Kanali Assimi Goïta (38) ambaye aliongoza mapinduzi ya kumng’oa madarakani Rais Ibrahim Keïta.
Baada ya mapinduzi ya Guinea, Kanali Doumbouya alisema askari wake wamechukua uongozi na walimedhamiri kumaliza ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya uliokithiri nchini humo.
Rais Condé alichaguliwa katika uchaguzi uliokumbwa na utata kuongoza kwa muhula wa tatu licha ya maandamano ya ghasia mwaka jana.
Leave a comment