Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Hukumu kesi ya Sabaya hadi tarehe 15 Oktoba
Habari MchanganyikoTangulizi

Hukumu kesi ya Sabaya hadi tarehe 15 Oktoba

Spread the love

 

HUKUMU ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili iliyokuwa itolewe leo imeahirishwa hadi tarehe 15 Oktoba, 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Amalia Mushi maetoa taarifa hiyo leo 1 Oktoba, 2021.

Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, ambao wanadaiwa kuvamia na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha wa zaidi ya Sh. 2.7 milioni, katika duka la Mohamed Saad, tarehe 9 Februari 2021.

Shahidi wa mwisho upande wa utetezi, ambaye alitoa ushahidi wake, alikuwa ni Mbura, akiongozwa na jopo la mawakili wa utetezi, likiongozwa na Wakili Dancan Oola.

Baada ya ushahidi huo kufungwa, Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, aliiomba mahakama hiyo itoe siku saba kwa pande zote mbili, kuwasilisha majumuisho ya kesi hiyo kwa njia ya maandishi.

Hakimu Amworo alikubali ombi hilo na kutoa siku saba kwa pande zote mbili, kuwasilisha majumuisho hayo.

Kesi hiyo, ilisikilizwa mfululizo kuanzia tarehe 19 Julai hadi 24 Agosti 2021. Ni baada ya Sabaya na wenzake, kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo mhakamani hapo, tarehe 16 Julai 2021.

Aidha, tarehe 24 Agosti 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo alipanga tarehe 1 Oktoba kuwa siku ya hukumu baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili.

Sabaya alifikishwa mahakamani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kumsimamisha tarehe 13 Mei 2021 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili.

Sabaya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, anza safari ya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai, tarehe 28 Julai 2018 na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!