Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinana ataja kinachomkwamisha Samia kuleta maridhiano ya kisiasa
Habari za SiasaTangulizi

Kinana ataja kinachomkwamisha Samia kuleta maridhiano ya kisiasa

Abdulrahman Kinana
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana, amesema kinachokwamisha dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuleta maridhiano nchini ni mabishano kuhusu vipaumbele vyake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Kinana ametoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa pili wa kumuenzi Hayati Maalim Seif Sharif Hamad, jana Jumapili, visiwani Zanzibar.

“Hii sio kazi rahisi kwani ziko changamoto zinazotukabili ikiwa ni pamoja na kutofautiana katika utekelezaji wake, kubishana kuhusu vipaumbele vyake, kuwa na mawazo tofauti kwa namna ya kasi ya utekelezaji wake. Ni vyema wanasiasa nchini kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kila mmoja kuheshimu mawazo ya mwenzake licha ya tofauti za kimtazamo na kimkakati,” amesema Kinana.

Kinana amewaomba Watanzania wamuunge mkono  Rais Samia katika kuleta maridhiano na mageuzi kwenye siasa, kwa kuwa kazi hiyo si rahisi.

“Rais Samia amedhamiria kuleta maridhiano na mageuzi katika siasa na uendeshaji wa taifa letu, amesema pahala pengi, amezungumza mara nyingi, amekutana na makundi mbalimbali. Kazi hii ameianza na anaendelea nayo,” amesema Kinana na kuongeza:

“Rais ana lengo la kusimamia haki, kukuza na kuimarisha uhuru, kupanua wigo wa kuendesha shughuli za siasa katika nchi yetu na kuleta mageuzi katika uendeshaji wa Serikali kwa madhumuni ya kuharakisha maendeleo ya taifa letu na watu wake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!