February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kimbunga chamia Marekani, chaua watu saba

Spread the love

WATU saba wamefariki nchini Marekani na wengine zaidi ya 1000 hawana makaazi ya kuishi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katikati ya mji wa Texas nchini Marekani ambazo zimeambatana na kimbunga kiitwacho Hurricane Hurvey, anaandika Irene David.

Kimbunga hicho kimekumba jimbo la Houston nchini humo ambacho kimesababisha uhabifu huo. Rais wa Marekani, Donald Trump, leo anatarajiwa kutembelea maeneo hayo yaliyoathiriwa na mafuriko.

Shughuli za uokoaji mpaka sasa bado zinaendelea japo bado hali si shwari kutokana na mafuriko hayo kuendelea kuwa mengi kutokana na kimbunga hicho cha Hurvey.

Jambo hili litakuwa ni janga la kiasili kutokea kwa mara ya kwanza Trump aingie madarakani.

error: Content is protected !!