Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kesi zazidi kumuandama Donald Trump
Kimataifa

Kesi zazidi kumuandama Donald Trump

Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Marekani, Donald Trump ameshtakiwa mara ya tatu ndani ya miezi minne iliyopita, sasa anatuhumiwa kula njama ya kutaka kubadilisha matokeo ya uchaguzi. Anaripoti Maryam Mudhihir, MUM … (endelea).

Mashtaka hayo yanadai kwamba alikula njama na watu wengine sita ambao majina yao haya kutajwa, kwa kutaka kubadili matokeo ya uchaguzi. Trump ameamriwa kufika katika mahakama ya serikali kuu alhamisi.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa na Jaji wa Mahakama ya wilaya nchini Marekani Tanya Chutkan, aliyeteuliwa na rais wa zamani Barrack Obama.

Smith amesema anataka kesi hiyo katika taarifa, timu ya kampeni ya Trump imesema Trump amekuwa akifuata sheria kila mara na kuyataja mashtaka hayo kama ‘unyanyasaji’ wa kisiasa ule wa enzi za Ujerumani.

Trump amemsuta mwanasheria huyo maalum, akimuita kuwa aliyechanganyikiwa ma kumtuhumu kwa kile alichokiita shtaka bandia ili kuingilia uchaguzi wa rais.

Ameandika kwenye mtandao wake wa Truth social kuwa kwanini hawakuyafanya hayo miaka miwili na nusu iliyopita? kwanini walisubiri muda  huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!