October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Mbowe: Shahidi adai alipigwa kwa dk45 akiwa kichwa chini, miguu juu

Spread the love

 

MSHITAKIWA wa pili katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kupanda njama za ugaidi, Adam Kasekwa amedai mara baada ya kukamatwa Moshi mkoani Kilimanjaro, alipigwa kwa muda wa dakika 45. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (enedelea).

Leo Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021, Kasekwa ameanza kutoa utetezi wake katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Mbali na Kasekwa, wengine kwenye kesi hiyo ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema, Freeman Mbowe, Halfan Bwire Hassan na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kasekwa ambaye aliwahi kuwa komandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alikamatwa tarehe 5 Agosti 2020 pamoja na mwenzake Mohamed Ling’wenya.

Akiongozwa na wakili Peter Kibatala kutoa ushahidi wake, Kasekwa amedai tangu walipokamatwa hadi kusafirishwa hadi Tazara jijini Dar es Salaam, tarehe 7 Agosti 2020, hawakuwahi kupatiwa chakula chochote kituoni walipokuwa au njiani.

Alipoulizwa, kipigo alichokipata kilitumia muda gani, Kasekwa amedai dakika 45 ambapo alikuwa akipigwa kwenye magoti akiwa miguu juu kichwa chini na kumfanya ashindwe kutembea.

Amedai, alikuwa akitembea miguu ina muuma kama mtu aliyepigwa shoti.

Kasekwa anaendelea kutoa ushahidi wake…

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!