January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rayvanny atibua party Harmonize

Harmonize

Spread the love

 

KITENDO cha msanii wa Bongofleva kutoka lebo Wasafi Classic Baby (WCB) na mwanzilishi wa lebo Next Level Music, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ kutangaza kumtambulisha msanii wake leo kimedaiwa kutibua party kama hiyo iliyokuwa inatarajiwa kufanywa na hasimu wake, Harmonize. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya Ravanny kutangaza kumtambulisha Macvoice ilihali upande wa lebo ya Konde Music Worldwide iliyo chini ya Rajab Abdul maarufu kama Harmonize ikiwa tayari imejipanga kumtambulisha msanii wao Cheed.

Kutokana na hali hiyo, Harmonize ametangaza kuahirisha sherehe hiyo ambayo ilikuwa imepewa jina la Cheed day.

Kupitia ukurasa wake Instagram Harmonize amesema sherehe iliyotakiwa kufanyika leo tarehe 24 Septemba 2021, haitokuwepo tena.

“Siku zote mwenye subra bila shaka yupo karibu na Mungu, najua ni kwa kiasi gani mnamsubiri Cheed ila napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba, kwa sababu zilizopo kando ya uwezo wetu (Cheed day) haitokuwa tarehe 24 Septemba 2021.’’

Cheed alisainiwa Konde gang tarehe 11 Septemba 2020, akitokea Kings music lebo ambayo inamilikiwa na Alikiba.

Cheed alitia nanga Konde Gand akiwa na msanii mwenzie anayefahamika kwa jina la Killy lakini hadi sasa bado hajatoa ngoma yoyote ilihali mwenzie Killy tayari ngoma kadhaa.

Aidha, baada ya Harmo kuweka ujumbe huo wa kuahirisha utambulisho wa Cheed baadhi ya mashabiki wamepasua jipu kuwa Konde gang wameogopa upande wa pili wa Next Level Music ambayo ipo chini ya hasimu wake Rayvanny.

Mmoja wa mashabiki hao amemjibu hivi Hamonize na kuungwa mkono na wenzie “Harmo acha uongo, sababu zipi wakati kila mtu anajua leo ni siku ya Rayvanny. Usitufanye watz wote wajinga.”

Ikumbukwe kuwa kumekuwapo na vita baridi kati ya manguli hao wawili yaani Rayvanny na Harmonize hasa ikizingatiwa wote wamelelewa na kukuzwa katika lebo moja moja ya WCB ili chini ya Diamond Platnumz.

Wakati Harmonize akiikacha WCB 2019 kuliibuka vijembe na maneno mengi huku msanii huyo akijiita Mwalimu wakati Rayvanny akijiita lecture yaani mhadhiri.

error: Content is protected !!