Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ya Mbatia kupinga kung’olewa NCCR-Mageuzi yakwama mahakamani
Habari za SiasaTangulizi

Kesi ya Mbatia kupinga kung’olewa NCCR-Mageuzi yakwama mahakamani

James Mbatia
Spread the love

USIKILIZWA wa kesi Na. 18/2023 iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam na James Mbatia, kupinga kufukuzwa ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi, umekwama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ni baada ya Wakili wa wajibu maombi katika kesi hiyo (Bodi ya Wadhamini ya NCCR-Mageuzi), Hassan Ruwanya, kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kuiondoa kesi hadi rufaa waliyokata kupinga ufunguaji wake itakapotolewa uamuzi.

Wakili Ruwanya aliwasilisha ombi hilo leo tarehe 11 Julai 2023, mahakamani hapo mbele ya Jaji Abdi Kagomba, wakati ilipokuja kuanza kusikikizwa kwa njia ya mtandao.

Wakili Ruwanya aliieleza mahakama hiyo kuwa, wateja wake wamefungua rufaa Na. 512/2023, kupinga uamuzi uliotolewa na Jaji Leila Mgonya wa kutupilia mbali kesi Na. 17/2023 iliyofunguliwa na Bodi hiyo kupinga maombi Na. 4/2023 yaliyofunguliwa na Mbatia.

Mbatia alifungua maombi hayo kuomba kibali cha kufungua kesi ya kuomba mapitio ya kimahakama dhidi ya mchakato uliotumika kumfukuza NCCR-Mageuzi, akidai haukuwa halali.

Wakili Ruwanya alidai, wateja wake wamefungua rufaa hiyo kupinga uamuzi uliomruhusu Mbatia kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa NCCR-Mageuzi, kwa madai kuwa haukuwa halali.

Hata hivyo, Wakili wa Mbatia, Hardson Mchau, aliiomba mahakama itupilie mbali ombi hilo kwa madai kuwa lilishawahi tolewa uamuzi mahakamani hapo katika kesi za awali.

Wakili Mchau alidai, mahakama hiyo mbele ya Jaji Mgonya, alitoa uamuzi wa kumruhusu Mbatia kufungua kesi kwa kuwa hatua hiyo haiwezi kuamua Haki ya mtu yeyote.

Baada ya pande zote mbili kuwasilisha hoja hizo, Jaji Kagomba ameahirisha kesi hiyo Hadi tarehe 13 Julai 2023, kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Mwanasiasa huyo amefungua kesi hiyo kupinga uamuzi wa kufukuzwa NCCR-Mageuzi Septemba 2022, kwa madai kuwa haukuwa halali kwani hakupewa haki ya kusikilizwa, lakini pia mkutano mkuu uliofikia hatua hiyo haukuwa halali

Katika hatua nyingine, mahakama hiyo mbele ya Jaji Mussa Pomo, imeahirisha usikilizwaji wa kesi ya madai Na. 59/2023, iliyofunguliwa na Mbatia dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini na wenzake watano, akitaka walimpe fidia ya kiasi cha Sh. 10 bilioni, kufuata kumchafua jina lake kwa kumtuhumu fisadi.

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya waleta maombi kuwa katika kesi nyingine.

Mbali na Selasini, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni vyombo vya habari; Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, inayochapisha gazeti la Mwananchi. Wasafi Media inayomilikiwa na msanii wa bongo fleva, Nasibu Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz).

Kampuni ya Jamhuri Media Limited, inayochapisha gazeti la Jamhuri. Kampuni ya Global Publishers na Mhariri wa Gazeti la The Citizens.

Katika kesi hiyo, Mbatia anamshtaki Selasini kwa kuchafua jina lake baada ya kumtuhumu ameuza Mali za NCCR-Mageuzi na mambo mengine.

Anamtaka Selasini athibitishe tuhuma dhidi yake mahakamani hapo na kwamba akishindwa alimpe fidia ya kuchafua jina lake.

Kwa upande wa vyombo vya Habari, Mbatia anavishtaki kwa kuandika habari anazodai kwamba zimemchafua.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Jumatano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!