Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kenya kurusha satelaiti yake ya kwanza ya uchunguzi wa dunia
Kimataifa

Kenya kurusha satelaiti yake ya kwanza ya uchunguzi wa dunia

Spread the love

 

KENYA inajiandaa kurusha satelaiti yake ya kwanza kabisa ya uchunguzi wa dunia katika kile kinachoelezwa kuwa mafanikio ya kihistoria katika juhudi za uchunguzi wa anga la juu nchini humo. Yameripoti Mashirika ya Kimataifa … (endelea)

Nation-1 au Taifa-1 kwa Kiswahili, imeratibiwa kurushwa wiki ijayo kwa roketi ya SpaceX Falcon 9 kutoka kituo cha anga cha Vandenberg huko California.

Satelaiti hiyo imeundwa ili kutoa data ya uchunguzi wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya kilimo, usalama wa chakula na usimamizi wa mazingira, wizara ya ulinzi na Shirika la Anga la Kenya zilisema katika taarifa ya pamoja.

“Iliundwa kikamilifu na kuendelezwa” na wahandisi wa Kenya kwa ushirikiano na mtengenezaji wa anga ya Bulgaria, taarifa hiyo iliongeza.

Ujumbe kutoka Kenya unatarajiwa kusafiri hadi Marekani kwa ajili ya uzinduzi huo.

Misheni hiyo inaonekana kama hatua muhimu kwa uvumbuzi wa kisayansi wa Kenya.

Nchi hiyo inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa baada ya misimu mitano ya mvua kushindwa.

Mnamo 2018, Kenya ilizindua majaribio yake ya kwanza ya satelaiti ya nano kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!