Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wapania kuwanyoosha bungeni waliotajwa ripoti ya CAG
Habari za Siasa

Wabunge wapania kuwanyoosha bungeni waliotajwa ripoti ya CAG

Bunge la Tanzania
Spread the love

 

BUNGE la Tanzania, limeombwa kutenga muda wa kutosha kwa ajili ya kuwashughulikia baadhi ya watumishi wa umma waliotuhuma kwa makosa ya ubadhirifu katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/22. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo tarehe 4 Aprili 2023 na baadhi ya wabunge wakati wakichangia hoja ya azimio la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha demokrasia na kukuza diplomasia ya uchumi, bungeni jijini Dodoma.

Akizungumza katika mjadala huo, Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu, amemuomba Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kutoa dakika 20 kwa kila mbunge kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya namna ya kukomesha vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma, vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali.

“Ngoma iletwe bungeni hapa, tuonyeshe hali ya hewa kwamba tunamuunga mkono Rais kwa kweli ya dhati. Tumechoka, tulitegemea pamoja na mambo mazuri yanayofanywa lakini wapo watalaamu wasio wazalendo . Safari hii spika tunaomba dakika 20 kuchangia ili tutoe adabu isije ikajirudia tena,” amesema Tabasmu.

Tabasamu amesema mhimili huo haupitishi bajeti kwa ajili ya wezi, bali linapitisha bajeti iliyokuwa na fungu la fedha za miradi ya maendeleo ya watanzania.

Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, amewataka wabunge watumie vikao vya mhimili vinavyoendelea, kuwanyoosha watuhumiwa hao wa ubadhirifu wa fedha za umma.

“Rais ameshatekeleza jukumu lake yamebaki majukumu kwa bunge hili, mimi niwaombe katika muda tulionao hapa wa siku 88, tunatarajia kuona majibu kutoka serikalini yatakayojibu changamoto za kimfumo na upande wetu wabunge kazi yetu tuonyeshe wenzetu mlango wa kutokea,” amesema Prof. Mkumbo na kuongeza:

“Kazi hiyo duniani huwa haifanywi na Serikali, inafanywa na Bunge, tunatarajia bunge hili watu wote ambao rais amesema wapishe na hawajaona mlango, sisi tuwaonyeshe mlango katika miezi hii mitatu hilo ni jukumu letu la msingi.”

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Msukuma), amesema wanasubiri ripoti hiyo ya CAG iwasilishwe bungeni ili wawanyooshe watuhumiwa hao, kwa madai kwamba wakiachwa watahamishwa katika maeneo mengine kisha kuendelea na vitendo hivyo.

“Wabunge mnasema tuwaoneshe mlango, hakuna mtu anayeweza kutoka kwenye mafuta kwa njia ya hiari hayupo. Mtu anaiba huku nyie mnamhamisha mnapeleka halmashauri nyingine huku anaendelea na uchunguzi anatumia pesa zetu kugharamia kesi. Ngoja hii ikija humu hatutaki tena kupiga swaga maana tumepiga mno,” amesema Msukuma na kuongeza:

“Kama huko Takukuru kuna Takukuru na kwenyewe kuundiwe tume kuchunguza, haiwezekani tumejadili sana mwaka jana, tunasubiri ngoma ije hapa tulale nao mbele.”

1 Comment

  • (xi) Mhe. WAZIRI Mkuu baada ya SERIKALI KUHAMIA DODOMA LINI VYOMBO VYA HABARI VYA ITV, EATV, TBC, AZAM TV, WASAFI TV, MWANANCHI VITAHAMIA DODOMA KWA LAZIMA.(TULIBUNI DSM HATUWEZI KUBUNI DODOMA)SWAHILI

    (xii) Dissertation (Confession Time):- Do high Unemployment Rate Influence Someone other Guys Creativity in solving PROBLEM, PRIDE, SOCIAL STATUS, WEALTH and Planning (TITANIC SOLVERS IN PARLIAMENT)?!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!