Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kanisa Katoliki Ngara lafungwa baada ya wasiojulikana kuvunja, kulinajisi
Habari MchanganyikoTangulizi

Kanisa Katoliki Ngara lafungwa baada ya wasiojulikana kuvunja, kulinajisi

Spread the love

KANISA Katoliki la Mt. Bernadetha wa Lurdi, lilioko Parokia ya Nyakati Buzirayombo, Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, limefungwa kwa muda wa siku 30, kwa madai ya kunajisiwa na watu wasiojulikana waliovunja na kunajisi sehemu yake ya kuhifadhia ekaristi takatifu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya kanisa hilo kufungwa imetolewa juzi na Makamu wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Father Ovan Mwenge.

Taarifa ya Father Mwenge inadai kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia tarehe 1 Septemba 2023, ambapo inadaiwa watu wasiojulikana walifanya kufuru baada ya kuvunja ukuta na kuingia ndani ya kanisa Kisha kuvunja Tabernakulo (sehemu ya kuhifadhia ekaristi takatifu).

Inadaiwa kuwa, wasiojulikana hao baada ya kuvunja Tabernakulo, walichukua ekaristi takatifu na kuondoka nayo, huku baadhi wakidondosha sehemu mbalimbali za kanisa hilo.

Kanisa hilo litafunguliwa baada ya kukarabatiwa na kutakaswa, huku waumini na wanajamii wakitakiwa kusali, kufanya toba na malipizi kwa Mungu ili abadilishe mioyo ya watu wenye Nia ovu kwa mambo matakatifu.

“Uharibifu huu uliotokea ni kufuru Kwa sakramenti ya ekaristi takatifu na umelitia najisi kanisa Kuu la Parokia ya Nyakati Buzirayombo. Pia, umeathiri kwa kiasi kikubwa utakatifu wa kanisa, kuvunja hadhi na heshima ya waumini na jamii kwa ujumla,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Kadri ya maelekezo ya sheria za kanisa kanuni namba 1211-1213 na kwa maelekezo ya Baba Askofu, Severine Niwemugizi, natangaza kufungwa kwa kanisa kwa muda wa siku 30. Baada ya marekebisho na ukarabati mdogo, kanisa litabarikiwa na kutakaswa ili liendelee kutumika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!