Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi shule ya East Africa Dodoma waonyesha vipaji
Elimu

Wanafunzi shule ya East Africa Dodoma waonyesha vipaji

Spread the love

KATIKA kukimarisha afya ya akili na mwili kwa wanafunzi shule ya Awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu jijini Dodoma, imeanzisha somo la mchezo wa karate. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Evarist Runiba, alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya darasa la saba ya shule hiyo.

Alisema michezo hiyo ni sehemu ya kuwasaidia kuimarisha afya za wanafunzi wao ili kufanya vizuri katika masomo yao na shunguli mbalimbali za kila siku.

“Shule yetu pamoja na kufundisha masomo mengine lakini pia tunafundisha lunga ya kichina na kifaransa lakin pia tunalo darasa la mchezo wa karate ambalo wanafnzi wote wanapata mafunzo wakiwa hapa shule”alisema

Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Alisema katika amchezo huo wa karate wanao walimu waliobobea katika mchezo huo hali ambayo itasaidia wanafunzi hao kuwa timamu kimwili na kiakili ili kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.

Mgeni rasmi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, alisema amefurahishwa na vipaji mbalimbali alivyoona kwenye shule hiyo.

Alisema ni vyema shule zingine ziige mfano huo kwa kutenga muda mzuri wa wanafunzi kucheza na kuimba.

Aidha, alisema kuna wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kama vilivyoonekana kwenye mahafali hayo na kwamba kama vipaji hivyo vikiendelezwa wanaweza kupatikana wasanii wakubwa nchini.

Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma

“Mnafanya vizuri sana na muendelee hivyo hivyo kwenye michezo na burudani kwasababu hawa wameonyesha vipaji vya aina yake natoa wito kwa shule zingine ziige,” alisema

Aidha, alisema michezo inawafanya wanafunzi wanakuwa na afya njema hali ambayo pia itachangia kufanya vizuri kwenye masomo na mitihani yao pia hivyo walimu wasione kama michezo ni kupoteza muda bila sababu.

“Mbalina masomo ya kawaida wapeni muda wa kucheza kuonyesha vipaji vyao, hawa lazima wapate muda wa kufanya mambo mengine yanayowapa furaha kama michezo,” alisema

Wanafunzi hao walionyesha umahiri mkubwa kwenye kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali hali ambayo iliwafurahisha wageni na wazazi waliofika kwenye mahafali hayo ambapo wengine walikuwa wakiwatunza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!