MKUU wa wilaya ya Kisarawe, Fatuma Almas Nyangasa amesema amefarijika na kasi ya uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Pwani (Corefa) chini ya Mwenyekiti wake Robert Munisi na Katibu mkuu wao, Mohamed Masenga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha michezo wilayani humo jana kwenye uwanja wa Bomani na kuudhuriwa na vijana zaidi ya 258, mkuu wa wilaya huyo alisema “Nimefarijika kuona wilaya ya Kisarawe inakuwa kimichezo kama ilani ya CCM na serikali yake ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyochagiza maendeleo ya michezo nchini hususani mpira wa miguu.”
Alisema Kisarawe watafanya makubwa katika kufanisha watoto wanakuwa wazuri kielemu na wenye vipaji hatakikisha anashirikiana na corefa pamoja na chama cha soka wilaya ya kisarawe(kidifa) kuendeleza na kukuza mpira wa miguu wilayani humo na kuwataka wadau kuwaunga mkono corefa kitimiza malengo yao.
Leave a comment