Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Kampuni, taasisi Arusha zakoshwa na huduma ya NBC Connect
Biashara

Kampuni, taasisi Arusha zakoshwa na huduma ya NBC Connect

Spread the love

TAASISI na kampuni wateja za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mkoani Arusha, wameipongeza benki hiyo kwa kuwapelekea huduma ya malipo kidigitali inayojulikana kama NBC Connect inayosaidia kuokoa muda na kuongeza ufanisi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Baadhi ya wateja walioalikwa katika uzinduzi wa huduma hiyo mkoani Arusha leo tarehe 5 Julai 2023 wamesema NBC connect itaziwezesha taasisi zao kufanya malipo  kwa njia ya usalama na bila kulazimika kufika kwenye matawi ya benki jambo ambalo litasaidia kuokoa muda.

Naibu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, David Lyamongi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ilifanyika jijini Arusha.

 NBC Connect, ni huduma ya kisasa ya kidigitali kwa makampuni na taasisi mbali mbali, ambayo huwezesha huduma salama za kibenki kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa njia ya mtandao.

Akizungumzia huduma hiyo, Joseph Buko kutoka kampuni ya Rhotia Valley amesema pamoja na kusaidia kuokoa muda, mfumo huo wa malipo kidigitali utaongeza ufanisi kwa kuwa unaruhusu kufanya miamala mingi kwa wakati mmoja na kwa ufanisi.

Mkuu wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi wa NBC, James Metairon akielezea namna huduma ya NBC Connect inavyoweza kurahisisha ufanyaji wa miamala kidigitali kwa wateja wa benki hiyo katika Hafla ya Uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika jijini Arusha


“Tunaishukuru benki ya NBC kwa kutulea huduma hii nzuri. Kulingana na mawasilisho yao kwetu, ni wazi kuwa itatusaidia sana kuokoa muda na muhimu zaidi, kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za kila siku,” amesema.

 Mteja mwingine aliyejitambulisha kama Yusuoh Zege kutoka University of Arusha ameishukuru benki ya NBC kwa kuja na huduma hiyo ya kibunifu na kuongeza kuwa inaonyesha namna ambavyo benki hiyo inawafikiria na kuwajali wateja wake ambao ni taasisi binafsi na za serikali.

 Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa wateja wakubwa, James Metairon amesema, “Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa  Arusha.
“Mfumo huu wa kibenki wa kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na kukidhi mahitaji  yao. NBC Connect itawawezesha wateja wetu wenye makampuni na taasisi mbali mbali kufanya huduma za kibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo.”

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ilifanyika jijini Arusha.

Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, NBC Connect itatoa usaidizi binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo mameneja wetu wanapatikana ili kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao nakutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia huduma hilo kwa ufanisi.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa Arusha wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya kwenye namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika  kuwa wateja wetu watafaidika nayo kwa kiasi kikubwa , “ameongeza.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu msaidizi Tawala Mkoa wa Arusha, David Lyamongi ameishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kibenki.

“Uzinduzi wa NBC Connect Arusha unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kufikia taasisi mbali mbali  na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Benki ya NBC inasifika kwa dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma Marathon zinazohamasisha matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!