Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Global Education Link yatoa fursa vyuo vya nje sabasaba
Elimu

Global Education Link yatoa fursa vyuo vya nje sabasaba

Spread the love
WAKALA wa Elimu Nje ya nchi Global Education Link (GEL), imeendesha zoezi la kudahili wanafunzi vyuo nje ya nchi papo hapo kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye vuiwanja vya mwalimu Nyerere maarufu kama sabasaba. Anaripoti Mwandishi wetu…(endelea)

Meneja Mkuu wa GEL,  Regina Lema, amesema leo kwamba wameamua kwenda sabasaba kwaajili ya kuwadahili hapo hapo wanafunzi waliohitimu kidato cha sita wanaotaka kwenda kusoma vyuo vikuu nje ya nchi.

Alisema pia wanadahili wanafunzi waliomaliza shashahada ambao wanataka kwenda kusoma kwenye vyuo vikuu vinavyopatikana nje ya nchi.

“Kwa sasa tunadahili wanafunzi wanaotaka kwenda kuanza vyuo vikuu nje ya nchi kuanzia Septemba mwaka huu na hapa tunasajili mwanafunzi ndani ya saa 24,” alisema

“Wanaofika hapa tunawapa ushauri wa bure kuhusu taaluma wanazotaka kusomea na vyuo ambavyo vitawafaa na kozi zao na tunawaonyesha fursa zilizopo za ufadhili katika vyuo mbalimbali,” alisema

Regina aliwataka wahitimu wa kidato cha sita kuchangamkia fursa ya kwenda kwenye maonyesho ya saba saba na kutembelelea banda la Global Education Link ili kuangalia fursa mbalimbali zinazopatikana.

“Ukingia tu viwanja vya sabasaba kuna njia inakunja kushoto unaenda nayo juu tuki jirani na TRC na Chuo Kikuu Dodoma kwa hiyo hii ni fursa ya kipekee kwa wahitimu wa kidato cha sita wanaotaka kwenda nje ya nchi kwa masomo,” alisema Regina.

Kuhusu mikopo kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi, Regina alisema Global Education Link wanakopesha mzazi ambaye anapaswa kurejesha ndani ya miezi nane baada ya mtoto wake kupata udahili na kwenda nje ya nchi.

Wanafunzi wakipata huduma ya kusoma vyuo vya nje kutoka kwa maofisa wa wakala wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) walipofika kwenye banda hilo katika viwanja maonyesho ya biashara ya kimataifa vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Alisema mikopo hiyo haina riba kwamba mzazi anaweza kukopeshwa hadi shilingi milioni 10 na kwamba iwapo atakamilisha taratibu atapata mkopo huo ndani ya saa 24.

Regina alisema kila mwaka wanadahili zaidi ya wanafunzi 700 wanaokwenda kusoma nje ya nchi na kwamba wamekuwa wakifuatilia maendeleo yao hadi wanapohitimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!