Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati za Bunge mguu sawa Bunge likianza 29 Agosti
Habari za Siasa

Kamati za Bunge mguu sawa Bunge likianza 29 Agosti

Spread the love

Bunge la Tanzania limesema, vikao vya kawaida vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza kufanyika Jumatatu tarehe 14 hadi 25 Agosti 2023 Jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya  Mkutano wa 12 wa Bunge utakaonza  tarehe 29 Agosti 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Bunge leo Jumapili na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa imesema Kamati tano zitatangulia kuanza vikao.

Imesema nne kati ya hizo zitaanza vikao tarehe 7 Agosti 2023 na Kamati moja ya Bajeti itaanza tarehe 10 Agosti 2023.

Imefafanua kuwa shughuli za kamati katika kipindi hicho zitakuwa ni: -Uchambuzi wa Miswada miwili ya Sheria utakaofanywa na Kamati mbili: Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Bajeti;

Pili ni uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge na tatu ni chambuzi wa Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa na CAG kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2022

Nne ni uchambuzi wa Taarifa za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa lengo la kuliwezesha Bunge kufuatilia ufanisi na tija kwa Mitaji ya Serikali kwenye mashirika mbalimbali na taasisi; na mwisho ni uchambuzi wa Taarifa za Utendaji za Wizara kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza jukumu la kuisimamia na kuishauri Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!