Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili
Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeitaka Serikali kudhibiti uuzaji holela wa dawa za asili zisizopimwa ubora, ili kulinda afya za wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 2 Februari 2023 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Stanslaus Nyongo, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na shughuli za kamati kwa 2019/2020.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Nyongo amesema kamati inaishauri Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR), kufanya utafiti dhidi ya dawa hizo ili kubaini ubora wake na kama ni salama kwa matumizi ya wananchi.

“Kupitia NIMR iweke mfumo wa kuhifadhi tafiti zote zinazofanyika nchini ili kujua na kutumia tafiti zote zinazofanyika kwa maslahi ya Taifa. Kuweka mpango mkakati wa kutenga fedha kutoka vyanzo vya ndani kwa ajili ya kufanya tafiti badala ya kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili wa nje ili kufanya tafiti nyingi zaidi,” amesema Nyongo akiwasilisha taarifa hiyo.

Aidha, Nyongo amesema, kamati hiyo ya Bunge inashauri NIMR iwekeze tafiti zaidi katika magonjwa yasiyoambukiza, kwa kuwa magonjwa hayo kwa sasa yanachangia asilimia kubwa zaidi ya vifo vya Watanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!