Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bilioni 215 zajenga miundombinu Kinondoni, mafuriko sasa basi!  
Habari Mchanganyiko

Bilioni 215 zajenga miundombinu Kinondoni, mafuriko sasa basi!  

Spread the love

ADHA ya mafuriko kwa wakazi wa Manispaa ya Kinondoni na Ubungo sasa imebaki kuwa historia baada ya jumla ya Sh bilioni 215.9 kutumika kujenga mifereji, mito na barabara za zege na lami kupitia Mradi wa Uendezaji wa jiji la Dar es salaam (DMDP). Anaripoti Gabriel Mushi …(endelea).

 Pia fedha hizo zimetumika katika usimikaji wa taa za barabarani zinazotumia nguvu ya jua, ujenzi wa njia za watembea kwa miguu, vyoo vya umma, masoko na sehemu za kupumzika katika maeneo mbalimbali ya Manispaa za Kinondoni na Ubungo.


Hayo yameelezwa leo tarehe 2 Februari 2023 na Mratibu wa Mradi huo katika Manispaa ya Kinondoni, Mkelewe Tungaraza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

Amesema lengo kuu la mradi wa DMDP ni kuiwezesha serikali kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kuibua fursa muhimu za uwekezaji ambazo hazijatumika ili kuboresha ukuaji na ustawi wa jiji la Dar es Salaam katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kujenga mwitikio wa dharura wa kukabiliana na majanga mbalimbali na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

 “Malengo mengine mahsusi ni; uboreshaji wa miundombinu ya barabara na mifereji ya maji ya mvua, kuimarisha uwezo wa taasisi katika kukusanya mapato. Pia kuimarisha uwezo wa watumishi katika usimamizi na ufuatiliaji wa miradi, kupunguza athari za mafuriko,” amesema.


Amesema jumla ya barabara za lami/zege zilizojengwa na kukamilika ni Km 70.21 pamoja na ujenzi wa Mto Sinza wenye urefu wa kilomita 8.50 huku mfereji Kiboko nao pia una kilomita 2.35.

“Tumeweka taa za Solar zilizosimikwa maeneo mbalimbali ni 1,939, tumejenga  mifereji mikubwa ya maji ya mvua iliyojengwa ni Km 28.93, maeneo ya kupumzikia mawili, vyoo vya umma vitatu, Ofisi na Maabara, vyote vikiwa na vifaa,” amesema.

 Alitaja baadhi ya barabara hizo kuwa zimejengwa katika maeneo ya Sokoni Makumbusho, Makanya- Tandale, Kisiwani – Kilimani, Simu 2000- Makumbusho, Kilongawima- Kyungi. External, Kisukuru, Majichumvi- Kilungule, Kilungule -Korogwe.

Aidha, amesema miradi hiyo ambayo ilianza mwaka 2016, ilikumbwa pia na changamoto mbalimbali ikiwamo kwenye mradi wa mto Sinza, ambapo baadhi ya nyumba ziliondolewa na mafuriko kabla ya utekelezaji wa mradi.

“Changamoto hii imesababisha wakandarasi kufanya kazi kwa ugumu kwa sababu baadhi ya maeneo huwa finyu na kusababisha malalamiko mengi ya nyumba kupata nyufa kutoka kwa wananchi mradi unapotekelezwa.

Aidha, amesema kutokana na ujenzi wa mto Sinza, mifereji pamoja na mabwawa mawili yaliyojengwa eneo la SamNujoma kwa lengo la kupunguza kasi ya maji ya mto Sinza, sasa mafuriko katika eneo hilo ulikopita mto huo yametoweka.

“Kwa kiasi kikubwa kero ya mafuriko imepungua sana hasa ukizingatia kuwa kabla ya mradi maeneo kama Bwawani-Mwananyamala, Tandale, Sinza, Kilongawima na Mbweni yalikuwa yanakumbwa na adha ya mafuriko nyakati za mvua.

“Pia mradi huu umeweza kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu, umeboresha na kupandisha thamani ya makazi na ardhi, umeongeza usalama katika maeneo ya mradi kutokana taa za barabara lakini pia umependezesha Jiji.

WANANCHI HAWA HAPA

Wakizungumzia miradi hiyo, hususani ujenzi wa mifereji na mto Sinzani, Hussein Idrisa ambaye ni mkazi wa Sinza Mugabe amesema hapo awali hali ilikuwa mbaya kutokana na mafuriko lakini sasa wanalala kwa amani hata mvua ikinyesha.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Christopher Mwakatuma ambaye aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kurekebisha miundombinu hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!