Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar
Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the love

HOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar. hali hii imetokea ikiwa mamlaka ya China kuripoti kwamba wimbi la taifa la ugonjwa wa Covid -19 linakaribia mwisho. Chombo cha habari cha NTD News kililiripoti.

Mtandao wa GeoPolitica.inf unaripoti kuwa hospitali za majimbo ya kati ya China zilifurika kwa kile walichokieleza sera zisizofaa za Serikali ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) za sefuri watu pamoja na chanjo zinazodaiwa kuwa hazifai.

Licha ya kuwepo kwa sera ya kutokomeza Covid-19, lakini bado ilionekana virusi hivyo kuliathiri taifa hilo ambapo Shirika la Afya Ulimwenguni (W.H.O) limesema kuwa hatua hizo hazisaidii katika kupunguza idadi ya visa na kuathiri vibaya maisha ya watu.

Voices Against Autocracy (VAA) imeripoti kuwa Serikali ya China inapindisha idadi ya vifo nchini humo ili kuficha ukweli.

Inalipotiwa kuwa China ilitangaza vifo 60,000 vinavyohusiana na COVID viliripotiwa kati ya mapema Desemba na katikati ya Desemba, 2022. Idadi hiyo ni kubwa ikizingatiwa kuwa China iliripoti idadi ya vifo 5,000 tangu kulipuka kwa ugonjwa huo jambo ambalo liliibua mjadala ulimwenguni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!