January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Joe Biden amchefua Balozi Haiti, ajiuzulu

Balozi Daniel Foote

Spread the love

 

RAIS wa Marekani, Joe Biden amedaiwa kumchefua Mwakilishi wake maalumu nchini Haiti, Balozi Daniel Foote baada ya kukataa mapendekezo yake kuhusu njia bora ya kushughulikia suala la wahamiaji kutoka Haiti wanaokimbilia Marekani. Anaripoti Helena Mkonyi –TUDARCo … (endelea).

Siku chache baada ya Idara inayoshughulikia mambo ya nje ya Marekani, kukataa mapendekezo yake, jana tarehe 23 Septemba, 2021 Balozi huyo amemuandikia Katibu Mkuu wa Serikali wa Marekani Antony Blinken barua ya kujiuzulu wadhifa wake.

Balozi Foote amevieleza vyombo vya habari kuwa amejiuzulu kwa sababu wahamiaji zaidi ya 3000 wanaokimbilia Marekani wamerejeshwa Haiti bila kujali utu.

Joe Biden, Rais wa Marekani

Balozi huyo ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo Julai mwaka huu amesema licha ya kwamba Haiti ni nchi inayokabiliwa na majanga kama vile vimbunga, matetemeko ya ardhi huku hali ya kisiasa ikizidi kudorora baada ya Rais Jovenel Moise kuuawa, bado Marekani haionekana kuwajaliwa wahamiaji hao.

Aidha, kufuatia uamuzi huo Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imemkosoa Foote kwa kujiuzulu kwake katika kipindi kigumu ambacho Haiti inapitia.

Msemaji wa Idara ya Mambo ya nje ya Marekani, Ned Price  amekanusha madai ya wizara hiyo kutupa mbali mapendekezo ya balozi huyo lakini akaongeza kuwa Foote ameshindwa kuwa mvumilivu.

error: Content is protected !!