Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Michezo Nabi: Yanga itakuwa tishio Afrika, kesho tunachukua kombe
Michezo

Nabi: Yanga itakuwa tishio Afrika, kesho tunachukua kombe

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)
Spread the love

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametamba kuwa Yanga itakuwa tishio ndani ya Tanzania na Afrika kwa ujumla kutokana na wachezaji wazuri waliosajiliwa msimu huu. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Nabi ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Septemba 2021 wakati akizungumzia maandalizi ya dabi inayotarajiwa kupigwa kesho katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam dhidi ya Simba.

Amesema kitu pekee cha kuleta furaha kwa Watanzania ni ushindi katika mechi hiyo hasa ikizingatiwa Yanga tayari imetolewa katika mashindano ya kombe la klabu bingwa Afrika.

Aidha, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa na subira kwa muda wa miezi kadhaa ili timu hiyo ipate muunganiko mzuri.

Pamoja na hayo amesema kuna changamoto ya matumizi ya wachezaji 10 wa kigeni waliosajiliwa na Yanga hasa ikizingatiwa sasa Shirikisho la Mpira nchini – TFF limeweka sheria kuwa wachezaji nane pekee wa kigeni ndio wanapaswa kuwepo kwenye kikosi cha timu ndani ya uwanja.

“Lakini kati yao naamini kila mmoja atacheza kadiri anavyojituma kwenye mazoezi. Kiujumla ninawapatia mbinu lakini suala la kujituma kwao ndio kila kitu katika mchezo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!