March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la Kenya lakamata Warundi wanaotamani ugaidi  

Spread the love

JESHI la polisi nchini Kenya limewakamata watu wanne  raia wa Burundi  waliokuwa wakielekea Somalia kujiunga na kundi la kighaidi la Al-Shabab, anaandika Catherine Kayombo.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa jeshi, George Kinoti washukiwa hao waliokuwa wakifuatiliwa na maofisa wa kijasusi, walikamatwa katika kizuizi cha polisi mjini Isiolo kaskazini mwa mji mkuu wa Nairobi wakielekea mji wa mpakani wa Mandera.

Washukiwa hao wanadaiwa kuingia nchini Kenya kama watalii kupitia visa huru ya ushirikiano kati ya Burundi na Kenya.

Aidha, ubalozi wa Burundi mjini Nairobi utatoa taarifa kamili kuhusu watuhumiwa hao waliokamatwa baada ya kushauriana na mamlaka kuu ya Kenya.

error: Content is protected !!