Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Waitara ambana Naibu Spika atoe ushuhuda
Habari za Siasa

Mbunge Waitara ambana Naibu Spika atoe ushuhuda

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

MBUNGE wa Ukonga  Mwita Waitara (Chadema) amembana Naibu Spika, Dk.Tulia Akson na kumtaka atangaze kuwa anautambua uongozi wa gani wa wabunge wa CUF ndani ya Bunge, anaandika Dany Tibason.

Waitara alimbana Naibu Spika wakati akiomba mwongozi wa Spika ili kutaka lijua msimamo wa Spika wa kutambua uongozi halali wa viongozi wa CUF ndani ya Bunge.

“Spika,Masuala ya CUF ndani ya bunge yameleta kizungunkuti kila mmoja anajua kuwa leo hii Spika ametangaza kutambua uongozi ulioletwa na wabunge wanaotokana na upande wa pili licha ya kuwepo kwa mgogoro.

“Leo  tunataka Spika atoe mwongozo  wa Bunge linawatambua viongozi gani ili kuhakikisha mzozo huo unaisha badala ya kuwepo mzozo usioisha ili lijulikane moja “ alihoji

Hata hivyo,  Naibu spika amesema hawezi kutoa majibu ya mwongozo huo kwani anatakiwa kusikiliza vyema maelezo ya Spika juu kuwatambua viongozi wa Bunge wa CUF wanaotokana na kambi ya pili.

Awali Chama cha Wananchi (CUF), upande wa mwenyekiti Prof.Ibrahim Lipumba kilitangaza kuunda kambi yao  bungeni tofauti na iliyokuwapo inayoundwa na UKAWA.

Bunge lilielezwa kuwa  Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara,  Magdalena Sakaya ambaye ni mbunge wa Kaliyua aliwasilisha majina ya viongozi wapya wa chama hicho kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Katika majina yaliyowasilihswa kwa Spika wa Bunge ni pamoja na jina la mbunge wa Mtwara Mjini ambaye amechaguliwa kushika nafasi ya mwenyekiti wa wabunge wa CUF bungeni.

Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, aliwaambia wabunge leo bungeni kuwa ofisi ya Spika ilipokea orodha mpya ya viongozi wa CUF 8 Agosti, mwaka huu na kueleza kuwa chama hicho kinautambua uongozi huo kwa sasa.

Kwa sasa mwenyekiti wa CUF ni mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea ambaye anaunga mkono uongozi wa Maalim Seif na kupinga uongozi wa Prof.Lipumba.

“Mnamo Septemba 8, mwaka huu, ofisi ya Spika imepokea ripoti kutoka kwa Sakaya na kuonyesha mabadiliko yaliyofanywa na mkutano wa chama hicho Septemba 6, mwaka huu.

“Kulingana na mabadiliko mapya,  Nachuma anakuwa mwenyekiti wakati mbunge wa viti maalum Rukia Kassim Ahmed ni Katibu wa chama bungeni” alieleza Dk Tulia.

Hata hivyo, Mbunge wa Malindi Ally Saleh (CUF) alikataa mabadiliko hayo kwa kutumia nafasi ya kuomba mwongozo wa Spika.

Ally Salehe aliomba mwongozo wa Spika akisema kuwa wabunge wa chama hicho wakiwa zaidi 40 walichagua viongozi na kwamba walipoondoka wabunge nane kulibaki nafasi zilizowazi.

Amesema walishafanya uchaguzi wa kujaza nafasi hizo ikiwemo nafasi ya uenyekiti iliyoachwa wazi na Riziki Ngwali na walimchagua Mbunge wa Temeke, Abdalah Mtolea.

Akahoji   ni nani anayeamua kuhusu uongozi wa wabunge bungeni ni wabunge wachache ama walio wengi.
Pia alitaka kufahamu  kwa sababu wao wameshafanya uchaguzi inawezekana kuwa na uongozi juu ya uongozi.

Akijibu Dk Tulia amesema Spika amepokea taarifa ya viongozi hao, lakini hajapokea taarifa ya uchaguzi wa upande wakina Ally Salehe.

Amesema watakapoleta taarifa yao ndipo Spika ataamua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy...

error: Content is protected !!