Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Machafuko yakosesha watoto elimu DRC 
Kimataifa

Machafuko yakosesha watoto elimu DRC 

Watoto nchini Kongo
Spread the love

ASASI isiyo ya kiserikali nchini kongo imesema  watoto wengi zaidi wanakosa elimu kutokana na mgogoro na mfumo duni wa elimu wa nchi hiyo. anaandika Victoria chance.

Ripoti ya Baraza la Wakimbizi la Norway imebainisha kuwa  asilimia 92 ya watoto wenye umri wa miaka sita hadi 11 wamekosa elimu katika miji iliyokumbwa na machafuko ya Kalemie na Tanganyika.

Shule 900 zimebomolewa kutokana na kushamiri kwa machafuko katika mkoa wa Kasai katikati mwa Kongo DRC katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Asasi hiyo imetahadharisha pia kwamba nchi hiyo kubwa ya katikati mwa Afrika inakabiliwa na hatari ya kupoteza kizazi chake kijacho kwa sababu katika mwaka huu umetolewa mchango wa asilimia nne tu ya fedha za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya sekta ya elimu ya Kongo DRC.

Baraza la Wakimbizi la Naorway limeongeza kuwa watoto waliotimiza umri wa kwenda shule wanachangia zaidi ya asilimia 17 ya watu wapatao milioni 3.8 waliopoteza makaazi yao nchini humo katika  kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!