JAJI wa Mahakama moja katika jimbo la Florida nchini Marekani ameiondoa sheria ya uvaaji barakoa katika vyombo vyote vya usafiri nchini humo.
Jaji Kathryn Kimball Mizelle amesema kwamba sheria hiyo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona ni kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Jaji huyo aliyetoa uamuzi huo amesema amri ya kuvaa barakoa iliyotolewa na Mamlaka ya afya nchini humo (CDC) ilivuka mamlaka yake.
Uamuzi wa Jaji huyo unaenda kinyume na agizo la Rais wa Marekani, Joe Biden aliyesisitiza na kukazia amri hiyo ya CDC ili kukabiliana na janga la maambukizi ya virusi hivyo vya Corona.
Wamarekani walikuwa wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa kwenye ndege, treni na mabasi. Amri hiyo ilikuwa imeongezwa hadi mwezi Mei.
Hata hivyo, Ikulu ya White House na wizara ya haki zinaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo.
Leave a comment