Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hapatoshi uchaguzi ngome vijana ACT-Wazalendo, wajitosa kumng’oa Nondo
Habari za Siasa

Hapatoshi uchaguzi ngome vijana ACT-Wazalendo, wajitosa kumng’oa Nondo

Spread the love

JOTO la uchaguzi ndani ya Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, limezidi kupanda baada ya makada wake machachari kujitokeza  kutaka kumng’oa Abdul Nondo, kupitia Uchaguzi Mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Februari mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hadi sasa vijana wa ACT-Wazalendo wenye ushawishi mkubwa waliojitokeza kuisaka nafasi ya uenyekiti wa Ngome ya Vijana, ni Mhandisi Ndolezi Petro na Julius Massabo, huku Nondo mwenyewe akitangaza nia ya kutetea kiti chake.

Mhandisi Ndolezi ni Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa chama hicho.

Julius Masabo

Ametangaza nia hiyo jana tarehe 6 Februari 2024, akisema uongozi ni kupokezana vijiti; anajiandaa kuchukua kijiti hicho kutoka kwa Nondo.

“Muda wa kampeni tutazungumza mengi, lakini kwa uchache yaliyonisukuma ni dhamira na nia ya dhati ya kuwatumikia Vijana wenzangu na Watanzania kwa ujumla,” ameeleza Ndolezi.

Akaongeza: “Ikumbwe kuwa kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makazi ya 2022,  takwimu zinaonyesha wenye umri chini ya miaka 36 ni aslimia 77%, hivyo kwa kiwango hiki Vijana tunakila sababu ya kujipambanua na kuingia kwenye majukwaa yatakayotupa nafasi ya kupaza sauti zetu juu ya changamoto tunazozipitia.”

Kwa upande wake Massabo, kupitia ukurasa wake wa Twitter akitangaza nia hiyo, amesema amechukua uamuzi huo ili kuimarisha ngome hiyo kwa kuwa vijana ndio msingi wa taasisi imara ya chama na nchi.

Petro Masabo

“Kwa kulitazama kwa picha kubwa ya nchi yetu, imani kubwa ya watanzania kwa chama chetu na kwa kuongozwa kwa misingi ya kizalendo, leo naomba niutangazie umma wa watanzania, wanachama wenzangu na vijana wa chama chetu kwamba nitagombea uenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa,” ameandika Massabo.

Massabo ambaye ni Naibu Kivuli wa Viwanda na Biashara wa ACT-Wazalendo, amesema vipaumbele vyake atavitangaza baada ya kuchukua fomu tarehe 14 Februari mwaka huu.

Katika kinyang’anyiro hicho amejitokeza Rukaiya Nasir,  ambaye ni mwanamke pekee kwenye kuwania kiti hicho kwa waliojitokeza kutia nia mpaka sasa.

Naye Marijani  Ndandavale Mwenyekiti wa ACT Mkoa wa Mtwara, pia Naibu Waziri Kivuli Wizara ya maji ya ACT Wazalendo ametia nia ya kugombea nafasi hiyo Katika kinyang’anyiro hicho amejitokeza Rukaiya Nasir ambaye ni mwaname pekee kwenye kuwania kiti hicho kwa waliojitokeza kutia nia mpaka sasa.

 

Rukaiya Nasir

Uchaguzi wa ngome hiyo unatarajiwa kufanyika tarehe 29 Februari 2024, ukitanguliwa na mdahalo wa wagombea utakaofanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Februari mwaka huu.

Nondo ambaye anamaliza muda wake, aliingia madarakani 2020, hivyo wajumbe wa ngome hiyo ndio wenye karata ya mwisho juu ya nani atakayeshika wadhifa huo kama watamrejesha madarakani au watachagua mwenyekiti mwingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!