Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Biteko aagiza wafanyabiashara, makundi maalumu kupewa kipaumbele ununuzi wa umma
Habari za Siasa

Biteko aagiza wafanyabiashara, makundi maalumu kupewa kipaumbele ununuzi wa umma

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameagiza Taasisi zote za ununuzi nchini (Serikali na Binafsi) kuhakikisha zinatoa kipaumbele katika manunuzi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi ili kukuza uchumi wa Watanzania na wazingatie kutoa kipaumbele kwa wafanyabiashara wadogo na makundi maalum. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema hayo tarehe 7 Februari, 2024 Jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ili kujenga ushirikiano unaolenga kuchochea ushiriki wa Wafanyabishara Wadogo, wa kati na Makundi Maalum katika masuala ya ununuzi wa umma.

“Kusainiwa kwa hati hii leo, kunazidi kuboresha mazingira ya Watanzania kushiriki kwenye uchumi wa nchi yao, hasa watu kutoka makundi maalum. Na haya ni  maelekezo ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha watanzania wote wanashiriki kwenye shughuli za kiuchumi, hivyo NEEC, PPRA, Taasisi nyingine za Serikali na Binafsi wawezesheni watanzania kushika uchumi wa nchi na muone fahari katika hili.” Amesema Dkt. Biteko

Kupitia hafla hiyo, Dkt. Biteko ameitaka PPRA kuzidi kuboresha huduma zake kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa rufaa zinazowasilishwa kwenye mamlaka hiyo hususani zile zinazohusisha waombaji wa zabuni kutoka makundi maalum ili kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi wa mtu mmoja mmoja na hatimaye Uchumi wa Taifa. Amezitaka mamlaka hizo kujikita zaidi katika uwezeshaji wa wananchi kwa kutoa elimu badala ya kubaki kuwa wadhibiti pekee.

Ameziagiza NEEC na PPRA kufanya tathmini na kutoa tuzo kwa watoa huduma wanaofanya vizuri katika uwezeshaji wa makundi maalum suala litakalochagiza ushindani miongoni mwa watoa huduma na hatmaye kukuza Uchumi.

Amesema makubaliano hayo yatatumika kama jukwaa la kuwahamasisha watu wa kundi hilo kushiriki na kuimarisha Uchumi wa mtu mmoja mmoja, kuimarisha wigo wa walipakodi na hivyo kukuza Uchumi wa nchi.


Ameipongeza PPRA kwa kuweka kanuni ya ushirikishaji makundi maalum kwenye manunuzi ambayo imeelekeza kuwa asilimia 30 ya zabuni zote zitolewe kwa washiriki kutoka makundi maalum ambao ni wanawake,vijana, Wazee na wenye mahitaji maalum.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama, amesema kusainiwa kwa hati ya makubaliano kati ya PPRA na NEEC ni ushahidi wa namna Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoamua kwa dhati kushikirisha makundi ya watu maalum kwenye uchumi na ujenzi wa Taifa.

Ameeleza kuwa, makubalinao hayo yataongeza ushiriki wa makundi maalum kwenyenunuzi ya umma na hii itaongeza uwezo wa watanzania katika uzalishaji malighafi na bidhaa pamoja na utoaji wa huduma ndani ya nchi.

Amesema kuwa, katika suala hilo la watanzania kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa, Ofisi anayoisimamia itaendelea kuisimamia NEEC ili iendeelee kuratibu utekelezaji wa sheria na hasa zile zinazohusu ushiriki wa watanzania kwenye miradi mbalimbali na kujenga uchumi wa nchi.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa, kusainiwa kwa hati hiyo kutaondoa mapungufu yaliyokuwa yakijitokeza kwenye masuala ya ununuzi wa umma hasa kwa watu wenye makundi maalum hivyo baada ya kusainiwa kwa hati hiyo utekelezaji wake utaanza mara moja.

Amesema siku zote Serikali inalenga katika kuwawezesha wananchi kiuchumi hali itakayoongeza walipakodi na hasa kwa watu wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi na wenye uwezo badala ya wananchi wa hali ya chini.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Baadhi ya Naibu mawaziri, Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri wa Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz, baadhi ya Wabunge na  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!