Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge (WMA)
Habari Mchanganyiko

Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge (WMA)

Spread the love

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewahamasisha viongozi wa vikundi 10 vilivyomo katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya  Burunge (WMA), kuhifadhi kumbukumbu zao za fedha kwa usahihi ili kuepusha migogoro itakayosababisha vikundi hivyo kuvunjika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara …(endelea).

Ameyasema hayo jana tarehe 7 Februari 2024 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu kwa viongozi wa vikundi hivyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya Chemchem Association inayofanya shughuli za uhifadhi katika Jumuiya ya Hifadhi Burunge iliyopo mkoani Manyara.

Amesema baadhi ya mambo yanayosababisha vikundi kuvunjika ni pamoja na kutotunza kumbukumbu kwa usahihi na kutumia fedha za kikundi bila utaratibu ambapo amewataka viongozi hao kutokuhifadhi fedha majumbani na badala yake kufungua akauti ya kikundi benki kulingana na sera ya fedha ya jamii ya mwaka 2019.

“Serikali inathamini sana vikundi vya kuweka akiba na kukopa kwani vikundi vinachochea maendeleo ya jamii hivyo viongozi wa vikundi mnapaswa kuwa waaminifu kwa pesa za kikundi ili kujenga imani kwa wanakikundi,” alisema Mkurugenzi huyo.

Awali, Meneja Mkuu wa Chemchem Association, Clever Zullu amesema wanajivunia kuwezesha vikundi hivyo kukopesheka na furaha yao ni kuona matunda ya uhifadhi yanaoongozwa na wananchi wenyewe kunufaika.

Amevitaja vikundi 10 vinavyosimamiwa na Chemchem Association kuwa ni Upendo -B, Marewa, Kigogoni, Datoga, Wacheda, Keja, Esinyati, Mdorii, Upendo -A na Mang’oo ambapo viongozi wa vikundi hivyo watapatiwa mafunzo ya siku tatu ili kuendana na Sera ya Community Microfinance ya 2019 ambavyo vitasajiliwa na kutambuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati.

Mkurugenzi wa Chemchem Association Fabian Bausch amesema umoja na mshikamano kati ya vikundi vya kuweka na kukopa vimewezesha kuwakwamua kiuchumi wakazi wa vijiji kumi vinavyozunguka Jumuiya ya Hifadhi Burunge.

Amesema wakati wanaanzisha vikundi hivi mwaka 2017 jamii haikuwa na uelewa mkubwa juu ya kuwa na vikundi vya kuweka na kukopa lakini kwa sasa dunia nzima inafahamu shughuli za uhifadhi zinazofanywa na kuwavutia wageni wengi wanaokuja kutali na kuongeza fedha nyingi za kigeni.

Kupitia fedha hizo Chemchem Association inatejesha kwa jamii kwa kusaidia katika sekta za elimu, afya na mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!