Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ujenzi wa bwawa la Kidunda wafikia 15%
Habari Mchanganyiko

Ujenzi wa bwawa la Kidunda wafikia 15%

Bwawa la maji Kidunda
Spread the love

Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bwawa la maji Kidunda mkoani Morogoro, unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), umefikia asilimia 15.

Mradi huo unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es salaam na Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, msimamizi wa mradi huo kutoka DAWASA, Mhandisi Christian Christopher ameeleza kuwa utekelezaji wa kazi mbalimbali unaendelea kama ilivyo katika mkataba wa mkandarasi.

“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na kusafisha barabara inayotoka Ngerengere hadi kijiji cha Kidunda zaidi ya kilomita 17 kwa ajili ya ujenzi, ujenzi wa kingo za mto, uchombaji wa eneo la bwawa, utayarishaji na upasuaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi, pamoja na kutengeneza tofali zinazotumika katika kujenga nyumba za watumishi.” ameeleza Mhandisi Christopher.

Mhandisi Christopher ameongeza kuwa ujenzi wa njia ya umeme toka Kidunda kwenda kituo cha kupooza umeme Chalinze ipo katika hatua za usanifu na ujenzi utaanza mara baada ya kukamilika kwa hatua hiyo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Christopher amebainisha kazi zilizokamilika tangu kuanza kwa mradi hadi sasa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za muda za mkandarasi, kufunga mtambo wa kusaga mawe, pamoja na kufanga mtambo wa kutengeneza zege.

Sambamba na kuhifadhi maji mengi yatakayotumika katika kipindi cha upungufu wa mvua, ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda unatajwa kuwa na faida nyingi ikiwemo uzalishaji wa umeme megawati 20 na kutengeneza ajira takribani 1,000.

Pia bwawa hilo litaboreshwa miundombinu ya barabara kutoka katika vijiji nufaika na mradi kama vile Ngerengere hadi kijiji cha Kidunda pamoja na kuchangia ukuaji wa shughuli za uvuvi pamoja na kuwa sehemu ya kivutio cha utalii.

Ujenzi wa bwawa la kidunda utakaogharimu kiasi cha zaidi ya Sh 300 bilioni, utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Juni 2023 hadi Juni 2026.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!