Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Jeshi Kongo lazima jaribio la M23
Kimataifa

Jeshi Kongo lazima jaribio la M23

Spread the love

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano lilizima jaribio la waasi wa M23 waliokuwa tayari wameukaribia mji wa Sake uliopo kilomita 27 kutoka Goma mashariki mwa taifa hilo la kati mashariki ya Afrika.

Vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa watu wasiopungua saba wamefariki katika mji huo baada ya bomu kuangukia eneo la makaazi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Raia waliobaki katika mji huo wamesema kuwa hali ya  tulivu umeanza kurejea kuanzia leo Alhamisi asubuhi.

Gavana wa kijeshi kupitia msemaji wake wa kiraia, Jymi Nziali aliyezuru mji wa Sake jana jioni ameviambia vyombo vya habari kuwa hali ni tulivu kwa sasa na kuwa wananchi wameanza kurejea majumbani.

Hata hivyo, ripoti zimesema mapigano mengine makali yanaendelea hadi mchana huu kwenye mji wa Kibumba wilayani Nyiragongo karibu kilometa 22 kaskazini mashariki mwa mji wa Goma ambako wapiganaji vijana wazalendo wanaoungwa mkono na jeshi la kongo wanakabiliana na M23.

Raia wa eneo hilo wameeleza kusikia milio ya makombora tangu asubuhi wakati vijana wazalendo walikuwa wakizilenga ngome za M23 kwenye vijiji vya Rwibiranga na Ruhunda mbali kidogo na Kibumba ya kati.

Waasi wa kundi M23 walirudi katika eneo hilo mwaka moja baada ya kuondoka  kwa kikosi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ilivyotakiwa na utawala wa Kinshasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!