Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Gari la Mbunge Ole Sendeka lashambuliwa kwa risasi
Habari za SiasaTangulizi

Gari la Mbunge Ole Sendeka lashambuliwa kwa risasi

Spread the love

GARI la mbunge wa Simanjiro (CCM) mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, limeshambuliwa kwa risasi eneo la Ndaleta, wilayani Kiteto wakati akiwa na dereva wake akielekea jimboni kwake Simanjiro. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea jioni ya leo Ijumaa tarehe 29 Machi 2024.

Amesema limetokea eneo la Ndaleta, Wilayani Kiteto wakati Ole Sendeka akiwa na dereva wake akielekea jimboni kwake Simanjiro.

“Ole Sendeka akiwa na dereva wake, gari lao lilishambuliwa kwa risasi ila hawakudhurika ni wazima kabisa,” amesema Kaimu Kamanda Mwakatundu huku akibainisha kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi na hakuna anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo.

Kaimu Kamanda amesema kwa sasa Ole Sendeka na dereva wake wapo Kituo cha Polisi Kiteto wakiendelea kuhojiwa kuhusu tukio hilo

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!