Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji
Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the love

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika Iftar iliyoandaliwa na Kampuni hiyo huku ikitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuendelea kuwaunga mkono sambamba na kuhimiza  kudumisha amani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Kampuni hiyo ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Fatma Abdallah imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa taasisi za umma na binafsi pamoja na wateja wa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah akisalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Iftar iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika Iftar hiyo alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Walid aliyewakilishwa na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Zailai Hassan Mkoyogore.

Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo Dk. Selemani Majige ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ni vema kila Mtanzania kwa nafasi yake kuendelea kuliombea Taifa sambamba na kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Tunafahamu kwa sasa tunaendelea na Mfungo wa Ramadhan pamoja na Kwaresima hivyo wakati tukiendelea na Mfungo ni vema tukaliombea Taifa letu lakini wakati huo huo kudumisha Umoja,amani na mshikamano,”amesema Dk Majige.

Amesisitiza kuendelea kudumisha amani katika nchini Kunafanya uchumi Wetu kuendelea kuimarika  na biashara zetu ziendelee vizuri.”Kulinda amani ni jambo kubwa kwani kama hakuna amani basi hata biashara haziwezi kufanyika vizuri.

“Hivyo kupitia mwezi mtukufu wa Ramadhan ni vema kuendelea kumuomba Mungu na kuendelea kumuombea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutuongoza na kudumisha amani katika taifa letu.”

Pia amewaomba Watanzania kuendelea kutumia mafuta  ya Puma Energy Tanzania pamoja na bidhaa zake zote huku akifafanua mafuta ya Kampuni hiyo yana ubora na viwango vya hali ya juu.

“Tunawaomba muendelee kutumia mafuta ya Puma  ili tuongeze faida na tukiongeza faida Serikali inapata gawio na inapotoa gawio zinapatikana fedha ambazo zinakwenda kuhudumia jamii katika maeneo mbalimbali,”

Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Temeke Sheikh Zailai Hassan Mkoyogole aliyemwakilishwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar  aliyekuwa mgeni rasmi, amesema kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan jambo kubwa ni kuzidisha wema kwa maana wanadamu ni wakosaji mbele za Mwenyezi Mungu.

“Binadamu anamkosea Mwenyezi Mungu kwa vitu vingi hivyo sasa ameleta Mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kutubu kwa yale yote ambayo ameyafanya.Hivyo kinachotakiwa katika mwezi huu ni kufanya yale yaliyomema na kurejea  kwake,”

Pia amesema Mwenye Mungu anapenda kuombwa ,hivyo ametoa mwito kwa watu wote kurejea kwa Muumba kuomba msamaha.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah amewashukuru wadau  waliojitokeza  katika futari hiyo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuwaunga mkono kwa kununua bidhaa za mafuta ya Kampuni hiyo.

Aidha amesema wao kama Puma Energy Tanzania wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali hasa katika kutekeleza matumizi ya  nishati safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la  kuendelea kutunza mazingira .

“Puma Energy Tanzania tunatambua mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na hasa kwenye suala la nishati safi hivyo tutaendelea kuaidia kwa lengo la kuhakikisha   mazingira yanalindwa na matumizi ya nishati  safi kwa watanzania yanakuwa kipaumbele.”

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu UDA- RT, Waziri Kindamba aliyeshiriki futari hiyo amewapongeza kwa kuandaa futari hiyo ni kuwaalika wateja wao ambao wanatumia vilainishi na mafuta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!