Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick
Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa ajili ya kuchunguza mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya askari polisi wanaolinda mgodi wa Barrick North, mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Ombi hilo lilitolewa katika mazishi ya Nyamonge Mseti, anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi tarehe 25 Machi 2024.

Akizungumza katika mazishi hayo, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Tarime Vijijini, Mlimi Zabroni, alidai kati ya Februari 2023 hadi Machi 2024, vijana takribani 10 waliuawa kwa kupigwa risasi katika maeneo ya mgodi huo.

Mlimi aliwataja vijana wanaodaiwa kuuawa na Polisi, akiwemo Jackson Nyamonge (28) aliuawa kwa kupigwa na risasi na polisi tarehe 12 Februari 2023. Musoma Machubu aliuawa tarehe 13 Julai 2023, Chacha Marwa (21 Septemba 2023), Mwita Augustino (26 Novemba 2023) na Lyoba Kisiri (17 Disemba 2023).

Samia Suluhu Hassan, Tanzania’s president, during an interview at Chamwino State House in Dodoma, Tanzania, on Monday, March 28, 2022. The second phase of negotiations with a group of companies led by Equinor ASA and Shell Plc for building the long-delayed LNG terminal are expected to conclude by June, Hassan said in an interview in her office on Monday. Photographer: Neema Irene Ngelime/Bloomberg

“Watu wanauawa, Mungu hakufanya hii dhahabu igeuke laana Tarime, leo vijana wanauawa lakini kuna ulegevu viongozi wetu tuliowateua hawasemi. Hili jimbo kuna mbunge kwa nini hazungumzii mauji Tarime, wenyeviti wa vijiji Tarime wameandika barua wanasema mgodi hauuwi vijana, sasa huyu ameuliwa na nani?” alidai Mlimi na kuongeza:

“Tunamuomba Rais Samia aunde tume aje aone wananchi wa Nyamongo wanavyouawa kwenye mgodi, polisi wanauwa vijana.”

MwanaHALISI Online imemtafuta Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, kupata maelezo yake juu ya hatua alizochukua kuhusu mauaji hayo yanayowakumba wapiga kura wake, ambaye amekiri uwepo wa matukio hayo na kwamba ameshachukua hatua kuwasiliana na mamlaka husika ili kutafuta mwarobaini wake.

“Nimeshafanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi na wakatoa taarifa ikiwemo majeruhi wakazungumza, baada ya hapo nikamuona Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara na mkuu wa mkoa hivyo wanafahamu vizuri na timu imetumwa kufanya uchunguzi kutoka ofisi ya Polisi na hata Mkuu wa Jeshi la Polisi analifahamu hili,” amesema Waitara.

Alipoulizwa nini kiini cha mauaji hayo, Waitara amedai ni hatua ya baadhi ya wananchi kutaka kuingia katika maeneo ya mgodi kinyume cha sheria huku wengine wakienda na silaha za jadi kitendo kinachopelekea pande zote mbili kutumia nguvu na hata kujeruhiana.

“Haya matatizo hayajaanza leo, mgodi una haki kama mwekezaji na wananchi wana haki ya kuishi kama raia wema. Waulize wakwambie kwa nini wameumizwa? Wakienda mgodini wanapambana na polisi kwa silaha ukikuta majeruhi ukiwaambia nenda polisi wanaogopa mkono wa sheria sababu na wao wana makosa,” amesema Waitara.

Mbunge huyo wa Tarime Vijijini, amesema wamiliki wa mgodi huo wamejitahidi kujaribu kukaa mezani na vijana wanaojishughulisha na masuala ya uchimbaji ili kuwajengea uwezo na hata kuwapa mitaji wakachimbe maeneo waliyoruhusiwa ili kudhibiti mvutano huo, lakini imeshindikana.

Waitara amedai kuwa, kiini cha mgogoro huo ni wananchi waliolipwa fidia ili wapishe mgodi kugoma kutoka, huku sababu ikitajwa wanagomea fidia kwa madai kuwa ni ndogo “unajua kabla fidia haijatolewa ilifanyika tathmini ya mali zilizopo lakini baadae ikagundulika baadhi ya wananchi baada ya tathimini waliongeza majengo na mazao hivyo mwekezaji kagoma kulipa fidia ya mali ambazo hazikuwepo.”

Mtandao huu ulimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime ili kujua hatua wanazochukua dhidi ya mauaji hayo, ambaye alimtaka mwandishi wa habari hii kumtumia meseji kisha baadae atatoa majibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!