Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Fedha za Uviko-19 kufikisha maji kwa wakazi 40,000 Dodoma
Habari Mchanganyiko

Fedha za Uviko-19 kufikisha maji kwa wakazi 40,000 Dodoma

Bomba la maji
Spread the love

 

WAKAZI wa Jiji la Dodoma wapatao 40,000 wanatarajiwa kunufaika kwa kuunganishiwa maji kutokana na fedha za mkopo wa masharti nafuu za UVIKO 19. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatatu tarehe 25 Julai, 2022,na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi ya maji katika jiji la Dodoma.

Amesema DUWASA ilipata fedha za UVIKO 19 DUWASA kiasi Cha shilingi bilioni 1.1 ambapo walipanga miradi ya kuifanya ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa Maji Safi.

Mhandisi huyo ameeleza kuwa eneo la Ntyuka Chimalaa hakukuwa na upatikanaji kabisa wa Maji lakini kupitia fedha hizo Mamlaka imejenga tenki la maji la lita 200,000.

Vile vile amesema kuwa, wameweka mtandao wa majisafi usiopungua kilomita tano,visima vitatu vilichimbwa huku akisema hivi sasa wananchi wanaunganishiwa maji.

Aidha Mhandisi Aron ameeleza kwamba mradi huo unaenda kuongeza maji katika eneo la Ntyuka Chimalaa kutoka asilimia 0 hadi asilimia 95.

Amezidi kufafanua kuwa fedha hizo pia zinaenda kutekeleza mradi mwingine wa Bahi Mjini ambapo wamechimba visima viwili ,wameweka mtandao wa majisafi wa kilomita 11 lakini pia wameweka tenki la maji la lita 200,000 .

Amebainisha kwamba mradi huo unaenda kuongeza maji kutoka asilimia 37 ya awali mpaka asilimia 90 mara baada ya mradi kukamilika.

Mhandisi huyo amesema mpaka sasa mtandao wa maji safi ni asilimia 65 huku watumiaji wa maji safi ni asilimia 82.

Kwa mujibu wa Mhandisi Aron ,kupitia fefha hizo pia Mamlaka imechimba visima Sita katika maeneo tofauti tofauti ikiwa ni mapambano ya kampeni ya jiji la Dodoma linalokua kwa kasi hasa maeneo ya pembezoni .

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wote kwa ujumla kutunza miundombinu ya maji,kutunza vyanzo vya maji kwa kupamda miti na kuhakikisha vyanzo vinaendelea kuwa salama,matumizi sahihi ya mifumo ya maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!