WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov amesisitiza kwamba nchi hiyo haihusiki kwa vyovyote vile na ongezeko la bei ya bidhaa muhimu duniani.
Ameongeza kwamba taarifa hizo zinaenezwa na nchi za Magharibi ili kueneza chuki dhidi ya nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya kimataifa … (endelea).
Waziri huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Julai jiiini Kampala, Uganda ambako yupo kwenye ziara yake ya nchi nne za Afrika.
Uganda ni nchi ya tatu kwenye ziara yake Afrika.
Sergey Lavrov amesisitiza kwamba Urusi haihusiki kwa vyovyote na ukosefu wa nafaka, ngano, mafuta na kupanda kwa gharama ya maisha kote duniani, kama inavyoripotiwa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.
Lavrov amedai kwamba mataifa ya Magharibi yamekuwa na hulka ya kuilaumu Urusi kwa kila baya.
Amesema gharama ya maisha zilianza kupanda kabla ya vita vya Ukraine, kwani zilianza katika kipindi cha janga la virusi vya Corona.
Licha ya kudai kwamba Urusi haihusiki na hali mbaya ya uchumi duniani, amedai kwamba vikwazo vya mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi ndiyo vimechangia hali hiyo, kwa kuvuruga usafirishaji wa
bidhaa muhimu.
Leave a comment