August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais wa zamani Burkina Faso aomba radhi mauaji ya Sankara

Blaise Compaore

Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaore ameiomba radhi familia ya kiongozi shujaa wa mapinduzi wa taifa hilo, Thomas Sankara kutokana na mauaji yake ya mwaka wa 1987. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Rais Compaore ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha bila kuwepo mahakamani jana tarehe 26 Julai, 2022, ametoa ujumbe huu; “Nawaomba wananchi wa Burkina Faso msamaha kwa vitendo vyote ambavyo ninaweza kuwa nilivitenda wakati wa uongozi wangu na hasa familia ya kaka yangu na ndugu Thomas Sankara.”

Compaore alitoa ujumbe huo uliosomwa na Msemaji wa serikali ya Burkina Faso, Lionel Bilgo.

Compaore alichukua madaraka katika taifa hilo la Afrika magharibi mwaka wa 1987 katika mapinduzi ya kijeshi ambayo yalimn’gatua na kumua kiongozi aliyekuwa anahudumu Sankara.

“Ninawajibika kwa hilo, na kujutia kutoka moyoni mwangu, mateso ya mikasa yote iliyowapata waathiriwa wote wakati wa mihula yangu kama kiongozi wa nchi na naomba familia zao zinisamehe,” ameongeza.

Compaore mwenye umri wa miaka 71, amekuwa akiishi uhamishoni katika nchi jirani ya Ivory Coast tangu alipofurushwa madarakani na maandamano makubwa mwaka wa 2014.

Alirudi Burkina Faso mwezi huu na kukaa siku kadhaa bila kukamatwa baada ya kiongozi wa kijeshi wa taifa hilo, Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba kumwalika kwa nia ya kuleta maridhiano ya kitaifa.

error: Content is protected !!