June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

EWURA yapeleka ‘zawadi’ vituo vya afya

Spread the love
KATIKA kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetoa msaada wa shuka 431 katika vituo vinne vya kutolea huduma za afya Jijini la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa tarehe 23 Juni 2021 jijini humo na Mhandisi Godfrey Chibulunje, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA wakati akizungumza na waandishi wa Habari.

Mhandisi Chibulunje amesema, shuka hizo zitapelekewa katika vituo vya afya vya Makole, Hombolo, Mkonze na Kikombo.

“Hii ni wiki ya Utumishi wa Umma na leo ndio Kilele cha maadhimisho yake, hivyo EWURA tunaadhimisha siku hii kwa kutoa msaada kwenye vituo vya afya vya jiji la Dodoma kama mchango wetu katika kuboresha huduma za afya,” amesema Chibulunje.

Dk. Endrew Method, Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo wa shuka, aliwashukuru EWURA na kuwaomba kuendelea kujitoa kusaidia katika maeneo mbalimbali ya afya.

Amesema, si mara ya kwanza kwa EWURA kusaidia na kwamba, kuna wakati walisaidia ambazo zilipelekwa kwenye huduma ya mama na mtoto.

“Katika Kituo cha Afya Makole, takribani wakina mama 120 wanajifungua kila wiki, hivyo tunapoboresha huduma tunalenga kuisaidia jamii,” amesema Dk. Method.

error: Content is protected !!