May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ni Uingereza dhidi ya Ujeruman robo fainali Euro

Kikosi cha England

Spread the love

 

MARA baada ya kukamilika hatua ya makundi ya michuano ya Euro 2020, hatimaye michezo ya 16 bora itaanza kupigwa siku ya Jumamosi, tarehe 26 Juni, 2021, huku timu ya Taifa ya Uingereza itavaana na Ujeruman katika hatua hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo wa kwanza kwenye hatua hiyo utakuwa kati ya Wales dhidi ya Denmark, ukifuatia na Italia ambao watamenyana na Austria.

Siku ya Jumapili Uholanzi itashuka dimbani dhidi ya Jamhuri ya Czech na kisha baadaye ukifuatia mchezo utakaovuta hisia za watu wengi kati ya Ubelgiji na timu ya Taifa ya Ureno.

Hatua ya 16 pia itaendelea tena siku ya Jumatatu tarehe 28 Juni, 2021, kwa michezo miwili ambapo mechi ya kwanza itakuwa Croatia dhidi ya Hispania, huku mabingwa wa Dunia timu ya Taifa ya Ufaransa itamenyana na Uswisi.

Kikosi cha Ujerumani

Uingereza wao watashuka dimbani siku ya Jumanne tarehe 29 Juni, 2021, ambapo wataialika Ujerumani katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Wembley uliopo London, na mchezo wa mwisho kwenye hatua hiyo utakuwa kati ya Sweden dhidi ya Ukraine.

Robo fainai ya michuano hiyo, itaanza kupigwa tarehe 2 Juni 2021, ambapo mchezo wa kwanza utakutanisha mshindi kati ya Ufaransa na Uswiss na mshindi kati ya Croatia na Hispania.

Siku hiyo hiyo itapigwa robo fainali ya pili ambapo itakutanisha mshindi kati ya Ubeligiji na Ureno atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Italia na Austria mchezo utakaopigwa kwenye jiji la Munichen, Ujerumani.

Robo fainali ya tatu, itapigwa siku ya Jumamosi ambao itakutanisha mshindi wa mchezo kati ya Uholanzi na Jamhuri ya Czech na mshindi katika mchezo wa Wales na Denmark, na hatua hiyo itafungwa kwa mshindi wa mchezo wa Sweden na Ukrain, atakayekutana na mshindi kati ya Uingereza na Ujerumani.

error: Content is protected !!