Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Majaliwa mgeni rasmi kilele cha dawa za kulevya
Habari Mchanganyiko

Waziri Majaliwa mgeni rasmi kilele cha dawa za kulevya

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

KASIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimishi ya kilele cha dawa za kulevya duniani tarehe 26 Juni 2021. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa tarehe 23 Juni 2021 na Antony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mbele ya waandishi wa Habari, maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini humo katika uwanja wa kumbukumbu ya sanamu ya Mwalimu Nyerere.

“Maonesho hayo yataanza siku ya siku ya tarehe 24 Juni. Katika maonesho hayo, kutakuwepo na mafunzo mbalimbali yanayoonesha madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya sambamba na makundi yaliathirika na utumiaji wa dawa hizo, ” amesema Mtaka.

Pia ameitaka jami hususani wakazi wa Dodoma kuhakikisha wanapambana na kuwa makini katika kuzuia uingizwaji wa dawa za kulevya kwenye maeneo yote ya mkoa huo.

Gerald Kusaya, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

“Wote tunajua na tumeona madhara makubwa ya utumiaji wa dawa za kulevya, tumepoteza nguvu kazi kubwa hususani vijana kwa hali hiyo ni lazima kupambana na Dodoma bila dawa za kulevya inawezekana,” ameeleza Mtaka.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya amesema, Tanzania ni kati ya nchi ambazo zinasimamia udhibiti wa dawa za kulevya.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinasheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, hivyo dawa zozote zenye kulevya haziwezi kukubalika wala kuruhusiwa kutumiwa au kilimwa.

“Pamoja na kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitoa mawazo ya kutaka kilimo cha bangi kiwepo, lakini ukweli haiwezi kukubalika na hiyo inatokana na kwamba, bado hakuna sheria ambayo inaruhusu kilimo hicho,” amesema na kuongeza:

“Katika mwaka 2019/2020 Tanzania imeweza kufikia asilimia 90 ya mapambano ya dawa za kulevya barani Afrika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!