Friday , 10 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango ampa maagizo mazito Balozi wa Tanzania-Uturuki
Habari za Siasa

Dk. Mpango ampa maagizo mazito Balozi wa Tanzania-Uturuki

Spread the love

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amemuagiza Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Balozi Idd Seif Bakari kuhakikisha anatekeleza diplomasia ya uchumi ikiwemo kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pia amemuagiza kutafuta wawekezaji hususani katika maeneo ya kipaumbele na kuwatafutia fursa wafanyabiashara na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Amemsihi balozi huyo kuendeleza na kukuza mahusiano baina ya Tanzania na nchi ya Uturuki kwa manufaa ya pande zote mbili.

Dk. Mpango ametoa maagizo hayo leo tarehe 30 Juni 2023 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi Bakari Jijini Dodoma.

Mbali na kumpongeza kwa kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenda kuiwakilisha Tanzania na watu wake katika taifa la Uturuki, Dk. Mpango amemuagiza kuhakikisha anakuwa na nyenzo muhimu zinazobeba vipaumbele vya nchi kama vile Dira ya Maendeleo ya Taifa, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020.

Makamu wa Rais amemuagiza Balozi Bakari kuhakikisha anashiriki katika mikutano mbalimbali itakayowezesha kujifunza, kueleza mazuri ya Tanzania pamoja na kutangaza utalii. Amesema ni vema kuendelea kuitafutia fursa na kuitangaza lugha ya Kiswahili,utamaduni, Sanaa na michezo ya Tanzania.

Amesema ni muhimu kwa Balozi huyo kufanya jitihada za makusudi kuifahamu vema nchi anayokwenda kuiwakilisha Tanzania ili kujifunza misingi ya ukuzaji wa uchumi wao na kuhamisha maarifa hayo kwa taifa la Tanzania.

Pia amemuagiza kuwaunganisha watanzania wanaoishi Uturuki ili waweze kuchangia vema maendeleo ya Tanzania.

Aidha, Balozi Bakari ametaja fursa zinazotokana na Ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki ikiwa ni pamoja na kuuza mazao nchini Uturuki kama vile pamba, kahawa, chai na tumbaku.

Amesema kutokana na Uturuki kuendelea kwenye sekta ya viwanda vya nguo ubalozi huo unatarajia kuongeza soko la mazao na kuhakikisha wawekezaji wa Uturuki wanawekeza Tanzania na kuongeza thamani ya mazao hapa hapa nchini.

Ameongeza kwamba Ubalozi unatarajia kuweka mkakati wa kukuza utalii kupitia Shirika la Ndege la Uturuki kwa kutangaza vivutio vya utalii walau wakati wa kuruka na kutua ndege hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

error: Content is protected !!