Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya NHIF yaita Watanzania kujisajili uanachama Sabasaba
Afya

NHIF yaita Watanzania kujisajili uanachama Sabasaba

Spread the love

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umewahimiza wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na waliotoka katika maeneo mbalimbali nchini kufika katika Banda la NHIF katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ili kupata huduma ya kusajili kuwa wanachama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 30 Juni 2023 na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Anjela Mziray ambaye ameeleza kuwa, kupitia Maonesho ya 47 yanayoendelea sasa katika viwanja hivyo, Mfuko unatoa huduma ya usajili wa wanachama kupitia mpango wa Vifurushi ambao unamwezesha kila mwananchi kujiunga na kunufaika kwa kuwa na uhakika wa matibabu.

Amesema kuwa mbali na usajili wa wanachama, Mfuko pia unatumia fursa hiyo kutoa elimu ya dhana ya bima ya afya na umuhimu wa kujiunga kabla ya changamoto za afya, kupokea mrejesho wa huduma na maoni ya uboreshaji wa huduma na kushughulikia changamoto mbalimbali walizokutana nazo wanachama.

“Tuko hapa Sabasaba katika Jengo la NHIF na mwaka huu tumekuja na huduma ya usajili wa wanachama, kuhuisha uanachama, kutoa usajili kwa waajiri na watumishi wao pamoja na elimu ya bima ya afya,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!