Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango akemea mivutano kati ya mawaziri na watendaji
Habari za Siasa

Dk. Mpango akemea mivutano kati ya mawaziri na watendaji

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais, Daktari Phillip Mpango, amewataka mawaziri kuepuka mivutano kati yao na watendaji wizarani, badala yake washirikiane kuwaletea maendeleo wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Februari 2023, Ikulu jijini Dar es Salaam, katika hafla ya uapisho wa viongozi walioteuliwa na Rais Samia, jana Jumanne.

“Watendaji bado tunaona changamoto katika wizara mbalimbali naamini mtakwenda mliangalie vizuri. Tumezungumza mara kadhaa Rais ameeleza hii mivutano kati ya naibu waziri, waziri na katibu mkuu haina tija. Mkae kama timu moja kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Watanzania,” amesema Dk. Mpango.

Miongoni mwa viongozi walioapishwa ni aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, aliyehamishiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Balozi Pindi Chana, ameapishwa kuchukua mikoba ya Mchengerwa katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Awali Balozi Chana alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Dk. Mpango amewataka mawaziri hao kuketi pamoja kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa kazi walizofanya kwenye wizara zao za awali.

“Wizara ya Maliasili ina historia kidogo, ina mafunzo mengi ni kati ya wizara ambazo zimekuwa na mawaziri wengi mojawapo ni hiyo ambayo ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu. Mchango wake katika fedha za kigeni na ajira ni kubwa sana , mmepewa dhamana kubwa kuhakikisha inaendelea kukua na kuchangia maendeleo ya nchi yetu,” amesema Dk. Mpango na kuongeza:

“Vilevile sekta hiyo bahati mbaya sana ina vishawishi vingi, nina uhakika Pindi atakudokeza mengi aliyoona kwenye kipindi chake. Nadhani umejiepusha na vishawishi hivyo kama kwenye vitalu na mengineyo.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!