MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangya Bangu amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo kumeonesha kuwepo kwa mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na wakulima kufurahia mfumo huo. Anaripori Danson Kaijage, Dodoma … (endekea).
Ameyaeleza hayo leo tarehe 15 Februali, 2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini hapa juu ya utekelezaji wa maendeleo katika mwaka wa fedha 2021/22.
Ameyataja mafanikio hayo ambayo yamepatikana toka kuanzishwa kwa mfumo huo wa Stakabadhi za Ghala ni pamoja na ongezeko la bei za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya Serikali kwa wastani wa asilimia 200% kutokana na urasimishaji.
Pia amesema mafanikio mengine ni ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 20 kwa mwaka, kichecheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni, upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
Sambamba na mafanikio hayo amesema kuwa pia kumekuwepo na ongezeko la mapato ya uhakika kwa Serikali Kuu na Serikali Mitaa na kukuza huduma za fedha vijijini.
Sambamba na hilo amesema kuwa tangu mwaka 2007 hadi sasa kilo bilioni 2.3 za mazao ya nafaka zimepitishwa na bodi hiyo na kilo hizo zinatokama na mazao 11 yanayolimwa hapa nchini.
Hata hivyo Bangu amesema kuwa bodi inashirikiana na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima kwa lengo la kuwafanya wakulima kupata mazao bora na salama ambayo yataweza kuingia katika soko la ndani na nje ya nchi.
Aidha ameeleza kuwa bodi hiyo kwa sasa imekuwa ikishiriki kupata mazao ambayo hayapo katika bodi ili nayo yaweze kuingizwa katika ghala huku wakiangalia ni jinsi gani ya kuanzisha maghala ya mazao ya kuoza kama vile maparachichi na nyanya pamoja na mazao mengine.
Ukiachana na mazao hayo ameeleza kuwa kwa sasa bodi inafikilia na ipo katika mazungumzo na wizara ya mifugo ili kuweza kuanzisha maghala ya mifugo kama vile ngozi sambamba na mazao ya nyuki.
Hata hivyo amezitaja changamoto kadhaa kuwa ni pamoja na kukosekana kwa elimu juu ya mfumo ambao unatumiwa na bodi hiyo kwa kuwepo na maneno ya uzushi juu ya mfumo.
Leave a comment